Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMBA ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote. Kwa mfano, mamba wa maji ya chumvi wanaopatikana Australia, wanaweza kung’ata kwa nguvu mara tatu zaidi ya simba au simbamarara.
Pia, taya la mamba lina uwezo wa hali ya juu, ambao unazidi ule wa ncha ya kidole cha mwanadamu. Hilo linawezekanaje ukizingatia kwamba ngozi ya mamba ina magamba?
Taya la mamba limefunikwa kwa maelfu ya viungo vya hisi. Baada ya kufanya uchunguzi, mtafiti Duncan Leitch aliandika hivi: “Kila neva imeunganishwa na fuvu la kichwa.” Mpangilio huo unalinda nyuzi za neva zilizo katika taya na kufanya sehemu fulani za taya ziwe na uwezo mkubwa wa kuhisi. Kwa sababu ya kuwa na uwezo huo, mamba anaweza kutofautisha mdomoni mwake kati ya chakula na uchafu. Hilo pia linamwezesha mamba jike kubeba watoto wake kwa kutumia mdomo bila kuwaua. Taya la mamba lina uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu na uwezo mkubwa wa hisi.
Aina ya mamba
Kuna aina nyingi ya mamba, kuna wale ambao huwashambulia wanadamu, hilo hutokea mara chache mno. . . mamba hawawezi kuorodheshwa kati ya wanyama ambao hula watu. (rejea kitabu Encyclopædia Britannica). Licha ya kwamba baadhi ya watu huwaona kuwa viumbe wenye sura mbovu na wanaotisha, watu wengine huvutiwa nao. Kuna aina tatu za mamba, wale wanaopatikana nchini India, yaani mamba wa maji ya chumvi, mugger na gavial.
Mamba wa maji ya chumvi
hawa ndio wanyama wakubwa zaidi wanaotambaa, wanaweza kufikia urefu wa meta saba au zaidi, na uzito wa kilo 1,000 hivi.
Usikose wiki ijayo…