27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Waendesha bodaboda wadhibitiwe barabarani

 WIMBI la madereva wa pikipiki maarufu bodaboda,   kujichukulia sheria mkononi bado linaendelea kutikisa maeneo mbalimbali nchini.

Madereva hao ambao wengi wao ni vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24, wamekuwa sumu   kwa wananchi wa kawaida  linapotokea jambo fulani,hasa ajali.

Isitoshe, mara nyingi ajali ambazo zimekuwa zikitokea husababishwa na vijana hao ambao wengi wao hawana elimu yaudereva, lakini wanapokuwa barabarani wao ndiyo hujiona wana haki zaidi kuliko  wengine.

Kitendo hicho husababisha watu wengi kuumizwa au kuharibiwa vyombo vyao vya usafiri, hasa magari,   linapotokea tatizo  la aina hiyo. Tumeshuhudia vurugu kubwa katiyao na wahusika wakichukua sheria mkononi.

Mara nyingi  tumeandika  kuhusu mwenendo huu kutokuwa mzuri na haupaswi kufumbiwa macho hata kidogo kwa sababu unavunja sheria za nchi.

Lakini pamoja na jitahada kubwa za kuwaelimisha vijana bado tatizo hilo limeendelea kuwa kubwalicha ya jeshi la polisi kuwakamata na kuwafikisha badhi yao mahakamani.  

Leo tumelazimika kuyasema haya baada ya wiki hii kutokea tukio la kusikitisha  eneo laManzese, Dar es Salaam, baada ya kundi kubwa la waendesha pikipiki haokujichukulia sheria mkononi  nakushambulia kwa mawe basi moja la mwendoharaka ambalo linadaiwa lilimgonga mwenzao aliyekuwa na abiria wawili.

Katika tukio hilo dereva wa pikipiki hiyo  alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na basi hilo.  Hapondipo waendesha pikipiki walipolishambulia basi hilo kwa mawe na  kuliharibu bila hata kujali abiria waliokuwamo.

Kundi jingine lilihamia kwa dereva wa basi ambaye naye alishambuliwa na  kuumizwa vibaya kwa    mawe.

Ndiyo  maana mpaka juzi, madereva 20 wa bodaboda walikuwa wametiwa mbaroni kutokana na uhalifu huo ambao kwa kweli haukubaliki.

Kimsingi matukio hayo  hutokea kutokana na matumizi mabaya ya barabara ya mwendokasi ambayo tangu kuzinduliwa kwake ilielezwa hakutakiwi  magari au pikipiki kupita humo.

Tunasema hivyo kwa sababu kila eneo katika barabara ya mwendokasi imewekwa alama ambayo mwendesha pikipiki au bajaji na hata mtembea kwa miguu anapaswakupita hapo. Tena kwa vyombo vya moto, bajaji na pikipiki kila wanapofika eneola kivuko cha waenda kwa miguu wanashauriwa kushuka na  kusukuma vyombo vyao, lakini  jambo hili limekuwa halifanyika kwa wengi wao wanapita maendeoe hayo wakiwa wanaendesha vyombo vyao! Hali hiyo imekuwaikichangia kwa kiasi kikubwa kutokea  ajaliambazo si za lazima.

Tunarudia kusisitiza na kuwaasa   waendesha pikipiki hao kwamba hakuna aliyeko juu ya sheria, kama limetokea jambo ni vema wakaachia vyombo vya dola vikafanya kazi yake.

Vyombo hivyo ndiyo vimepewa mamlaka kamili ya kushughulikiamatukio ya  kila aina. Hivyo waendesha pikipiki waache kujijengea ‘jamhuri yao’ na kuonekana muda wote wanaonewa!

Tunamalizia kwa kutoa rai tena kwa pande zote mbili,  madereva wa mabasi ya mwendokasi na pikipiki, kuheshimu alama za barabarani kuepukana na athari zinazoweza kutokea.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles