25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau watakiwa kuhamasisha wananchi kutokomeza TB

Na Janeth Mushi, Dar es Salaam
 
Wadau mbalimbali wa Maendeleo hapa nchini wametakiwa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuachana na dhana potofu ya unyanyapaa kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu nchini.

Hayo yamesemwa Mei 24, 2021 jijini Dar es Salaam na Mtaalamu Mbobezi wa masuala ya Kifua Kikuu (Utafiti na Tathmini), Dk. Zuweina Kondo katika warsha ya Kifua Kikuu, Jinsia na haki za binadamu iliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na sekta ya afya Afrika Mashariki (EANNASO) kwa kushirikiana na Tanzania TB Network.

Amesema ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni janga duniani ambapo takwimu za WHO mwaka 2020 zinaonyesha watu zaidi ya watu milioni 11.4 walifariki dunia kutokana na ugonjwa huo huku wagonjwa wapya waliougua ugonjwa huo wakiwa milioni 10 ambapo kati yao wanaume ni asilimia 56, wanawake asilimia 32 na watoto asilimia 12.

“Ugonjwa wa kifua kikuu ni janga na linatokana na dhana  potofu za imani za kunyanyapaa wenye kifua kikuu na serikali inakuwa na mikakati mbalimbali hasa kuwapa elimu kwa njia ya matangazo,kupitia vyombo vya habari pamoja na kushirikiana na wadau wakiwemo asasi za kijamii ili kufikisha ujumbe kwa jamii.

“Kikao kazi hiki ni maalum cha kuongelea masuala ya haki,jinsia na ambavyo kwa namna moja ama nyingine yanachangia watu kutokupata huduma za kifua kikuu.Takwimu zinaonyesha akina baba wanaugua zaidia kifua kikuu lakini akina mama wameoneakana hatujawafikia zaidia,tunaangalia sheria, tabia zinakinzana vipi kuhakikisha wananchi wanapata hizi huduma,” amesema Zuweina.

Mtaalamu huyo ameitaka jamii kutambua kuwa ugonjwa wa kifua kikuu unatibika na siyo ugonjwa wa kurithi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa EANNASO, Onesmus Mlewa amesema lengo la warsha hiyo iliyokutanisha wadau wakiwemo wataalamu wa afya,Majaji,Wanasheria na Waandishi wa habari ni kujadiliana namna ya kuendeleza mchakato wa kutokomeza ugonjwa huo na kuelimishana ili kupata viongozi ‘champions’ katika sekta mbalimbali.

“Ukiangalia kifua kikuu ni moja ambayo yamesumbua kwa muda mrefu,tukishirikiana na kuipa uzito unaostahili tutasaidia kupunguza maambukizi na kwani kutokana na ugonjwa huo kusambaa kwa njia ya hewa hivyo  tuko katika hatari kubwa mno kwani wanapozidi kuwa wengine na hatari ya kuambukziwa ni kubwa,”amesema Mlewa.

Upande wake, Mtaalamu wa Afya aliyebobea katika masuala ya Sayansi za Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Wilbard Muhandiki amesema hali ya ugonjwa wa kifua kikuu nchini siyo nzuri kwa sababu tumeendelea kuwa kati ya nchi 30 zenye maambukizi makubwa.

“Kwa sasa hivi tumepambana kidogo kutoka asilimia 65 mwaka 2015 hadi 81 sasa hivi  lakini bado tunakosa  asilimia kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu.Kwa mwaka tunakadiria  kuwa na wagonjwa 137,000 kwa mwaka sasa tumepata 81,000 hivyo kuna wagonjwa wengi hatujawafikia na wanaendelea kuambukiza wengine.

“Sababu za kukosa wagonjwa ni pamoja na kijografia nchi ni kubwa,wagonjwa walio wengi uwezo wa kifedha kuweza kuwafikia kila mahali lakini bado hatuwezi kufika kila mahali kwa hiyo tuna tatizo la kifedha,tuna tatizo la elimu kwa jamii watu wengi inawezekana hawajapata elimu za kifua kii na kuweza kufika katika vituo vya kutolea huduma hizo ili waweze kugundulika mapema na kupewa matibabu,”amesema Dk. Mhandiki.

Amesema serikali inafanya juhudi kubwa za kudhibiti ugonjwa huo kwa kuongeza vituo vya wagonjwa,kuhakikisha kunapatikana kwa dawa za ugonjwa kifua kikuu pamoja na kushirikiana na wadau wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles