Wadau wajadili mpango wa Blue Print

0
760

Mwandishi wetu -Morogoro

SERIKALI imewataka wadau wa sekta binafsi kuhakikisha wanarasimisha biashara zao ili waweze kupata matokeo chanya yanayofanywa katika muongozo wa uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara nchini.

Rai hiyo imetolewa jana mkoani Morogoro na Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS), Gervas Kaisi, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Baraza la kilimo Tanzania kwa kushirilikiana na Programu ya Kuimarisha Mifumo ya Masoko katika Mnyororo wa Thamani (AMDT).

“Tangu tumezindua Blue Print ni kweli Serikali imefanya maboresho makubwa hasa kwenye tozo ambazo zilikuwa ni kero kwa wafanyabiashara, lengo kuu ni kuhakikisha tunaboresha mazingira ya ufanyaji biashara, kwa sasa zaidi ya tozo 150 tumekwisha kuzitoa,

“Lakini pia hatua nyingi zinachukuliwa na Taasisi mbalimbali za Serikali za kuunganisha mifumo yake kwenye mtandao  ili iwe rahisi katika upatikanaji wa huduma na tayari kuna taasisi zimekwisha kutekeleza suala hilo,” alisema

Wadau hao wa sekta binafsi wametakiwa kuhakikisha wanaendelea kutoa maoni yao kuhusu muongozo huo ambao utekelezaji wake umaeanza mapema mwaka huu 2019 na kwamba ni muhimu mapendekezo hayo yakaendana na nini wangepata seriklai ifanye.

“Kama ukisema tozo ni muhimu useme aina ya tozo inayokukera ili tuwezekuifanyia kazi kikamilifu, lakini pia ni muhimu sana hata kama kuna kanuni inakukera katika biashara zako tuambie kwa kuitaja kabisa aina ya kanuni hiyo na serikali ni sikivu tutatekeleza,” alisema.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo, Omary Mwaimu, alisema wadau wa sekta binafsi hasa kilimo wana wajibu wa kurasimisha biashara zao ili kuendanda a utaratibu wa serikali.

Kwa upande wake Mtaalamu Mwelekezi na Utetezi kutoka Programu ya kuimarisha Mifumo ya Masoko katika Mnyororo wa Thamani  (AMDT), Tertula Swai, alisema mkutano huo umelenga kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya kilimo  kama muongozi unavyotaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here