24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

WADAU WAJADILI MPANGO KUENDELEZA HIFADHI ZA TAIFA

Editha Karlo, Kigoma

Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za taifa mbalimbali zilizopo nchini ili kujifunza na kujionea urithi na vivutio adimu vilivyopo kwenye hifadhi hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga amesema hayo leo wakati warsha ya siku moja ya wadau mbalimbali wa Mkoani Kigoma wa Hifadhi ya milima ya Mahale kilichokuwa kinajadili mpango kabambe wa miaka 10 wa kuendeleza hifadhi hiyo.

Amesema Mkoa wa kigoma umepata bahati ya kuwa na hifadhi mbili za taifa ikiwamo Mahale na Gombe hivyo lazima juhudi za kutangaza hifadhi hizo ziongezeke.

“Tunajua Hifadhi ya Mahale ina changamoto ya usafiri wa kufika kule kwani ili kufika inakulazimu kusafiri kwa njia ya maji kwa muda mrefu kutumia boti za kawaida, tunaomba mtuwekee boti ya mwendo kasi, tunafahamu TANAPA mnafanya kazi kubwa kuhakikisha watalii wanafika Mahale kwa njia ya barabara,” amesema Maganga.

Aidha, amesema mtu mmoja anapotembelea hifadhi ni sawa na watu 10 wametembelea kwani akitoka huko anakuwa balozi wa wengine ambapo pia ametaka kupitia sekta ya utalii lazima iendane na kauli mbiu ya serikali ya sasa ya Tanzania ya Viwanda.

“Hawa watalii kutoka nchi mbalimbali wanaokuja kutembea vivutio vyetu pia huwa wanaangali wapi pa kuwekeza tutumie fursa hizo za kuwashawishi waje kuwekeza nchini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,853FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles