25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Wadau waeleza madini yanavyotoroshwa kwenye matikiti maji, kabichi

Anna Potinus, Dar es Salaam

Wadau wa madini wameeeleza jinsi madini nchini yanavyotoroshwa kwenda nje ya nchi kupitia mipakani.

Wadau hao wameeleza hayo leo Jumanne Januari 22, Mkutano wa Kisekta wa Wizara ya Madini ulioshirikisha wadau mbalimbali wa madini, baada ya Rais John Magufuli kutoa nafasi kwa wadau hao kuelezea changamoto zinazowakabili.

Mmoja wa wadau wa madini kutoka mkoani Geita, amesema madini hayo hutoroshwa na watu kutoka nje ya nchi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwamo kuficha kwenye matikiti maji.

“Mtu anaweza akaiba dhahabu na kuweka hata kwenye ‘side mirror’, tikiti maji, kabichi, au tairi la spea, kwenye tikiti maji na kabichi anakata anaingiza kilo nyingi tu za dhahabu.

“Tukipata nafasi ya kuzungumza kwa utaratibu tutayasema haya yote, serikali inatoa taarifa ambazo sio sahihi ndiyo maana uliposema tujadili watu walipiga makofi.

“Pale Uwanja wa Ndege wa Mwanza, zile mashine ukienda na karatasi za namna fulani ukafunga madini unapita bila usumbufu wowote, nilienda kwenye kamati na tukakubaliana kwenda kuhakikisha na tulipofika ni sehemu moja tu ilionyesha kuna madini lakini sehemu nyingine hazikuonyesha,” amesema.

Naye Mwakilishi wa Tanzanite, alieleza changamoto inayowakabili ni mishahara baada ya ukuta wa Mirerani mkoani Manyara kujengwa kwani waliambiwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa mishahara na hilo limekuwa tatizo kwa wachimbaji wadogo.

“Kama sisi, tungekuwa tunaruhusiwa kuingia ndani ya ukuta kufanya biashara fedha ingeonekana, vijana hawaruki ukuta kutoka ndani bali wanaruka kutoka nje kuingia ndani kwaajili ya kuchimba madini kutokana na kuzuiwa kuingia bila kulipa.

“Tunawajua watu wanaotorosha madini ukituita nje ya kamera tuwataje, yanatoroshwa na wageni ambao ni Wachina na Wazungu, tunaomba vyombo vya dola vifuatilie,” amesema.

Kwa upande wake mmoja wa wachimbaji wa Almasi, amesema wanunuzi wa ndani wanashidwa kumudu ukubwa wa ada ya leseni hivyo anaomba kwa wazawa iwe Sh milioni moja na kwa wageni Dola 5,000.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles