25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wa elimu wataka mazingira wezeshi shuleni

Ramadhan Hassan, Dodoma

Wadau wa elimu nchini wameishauri serikali kuongeza idadi ya walimu kutokana na wanafunzi kuwa wengi kuliko walimu na kuweka mazingira yatayowezesha kupatikana kwa elimu bora.

Aidha, wameitaka kuongeza vifaa vya kufundishia na miundombinu ya kusaidia wanafunzi kusoma katika shule hizo.

Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Ten/Met, Ochola Wayaga amesema hayo leo Jumatano Desemba 11, katika ufunguzi wa mkutano wa 11 wa mwaka wa wadau wa elimu nchini.

Amesema licha ya kuwepo juhudi za   kuboresha elimu nchini kwa kuwa na sera ya elimu bila ada lakini bado kuna changamoto ambazo zinatakiwa kutatuliwa.

“Serikali inatakiwa kuangalia kwa umakini ubora wa elimu inayotolewa nchini kwa lengo la kupata wataalamu wenye ubora  katika siku za baadaye na ili kupata wasomi wazuri ni lazima kuangalia ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari na si kuangalia wingi wa wanafunzi waliopo mashuleni.

“Suala la ubora wa elimu ni muhimu kwa taifa kwani kama wanafunzi watakuwa na elimu ambayo si bora ni wazi kuwa taifa haliwezi kuwa na maendeleo yanayokusudiwa,” amesema.

Wayaga alisema mkutano huo wa siku tatu una mada kuu nne zikiwemo za kuangalia kiundani maendelelo ya watoto katika kupata elimu, elimu shirikishi kwa watu wenye ulemavu, elimu kwa wasichana na ubora wa vifundishio na mazingira ya kujifunzia.

Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo alipongeza mchango wa Mtandao wa Elimu Tanzania katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles