Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wamekutana katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), kujadili namna ya kuboresha elimu hiyo.
Wakijadili mradi wa Kituo cha Umahiri wa Tehama (Rafic) uliopo DIT, Mratibu wa Mradi huo unaofadhikiwa na Benki ya Dunia (IMF), Joseph Matiko amesema mradi huo utasaidia kuboresha elimu ya ufundi na Tehama ili kuzalisha vijana watakaotumika katika kusaidia mapinduzi ya viwanda.
“Wadau wa Tehama ni muhimu kujadiliana kuona namna gani mtatusaidia katika hatua mbalimbali za utengenezaji wa mitaala na namna gani tutakavyowashirikisha kwenye shughuli za uendeshaji.
“Katika mradi huo tutajenga jengo la kisasa, ununuzi wa vifaa vya kufundishia maabara vya kisasa, ofisi ya za walimu, maktaba na mabweni ya wanafunzi kutoka nje ya nchi na nyumba za kuishi wakufunzi wageni,” amesema Matiko.