24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau Haki za Binadamu watoa wito kwa Serikali kuhusu Katiba

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Jukwaa la Katiba (JUKATA) wametoa maoni na wito kufuatia msimamo wa Serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya uliotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Noumbaro katika mkutano wa wadau wa sheria ikiwemo mawaziri wastaafu uliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu Agosti 28, 2023.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari Agosti 29, 2023 katika Ofisi za LHRC makao makuu, Kijitonyama Anna Henga Mkurugenzi Mtendaji LHRC, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Katiba (Jukata) Bob Wangwe, Ananilea Nkya Mwenyekiti Jukata kwa pamoja wametoa wito kwa Serikali.

“Tupate Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kutoanza kutoa Elimu ya Katiba, Wito kwa Wadau Katika Mipango ya Katiba Mpya (Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali wa katiba kuna umuhimu wa kushiriki katika kupaza sauti zao ili kuzuia jaribio hili la kuturudisha nyuma kutofanikiwa,” amesema Henga.

Aliongeza kuwa ikitumika miaka mitatu kutoa elimu ya Katiba alafu ndiyo mchakato uanze baadaye itapeleka kuanza mchakato wa katiba mpya miaka minne ijayo na kupelekea kutofika tena kwenye uchaguzi wa 2030 bila katiba mpya.

“Kutoa elimu ya Katiba mpya ni kurudi nyuma, tunaona kama hatua hii itakua na matokeo hasi katika matumizi sahihi ya fedha za wananchi kwa kuzingatia ukweli kwamba msimami huu wa serikali hauendani na mahitaji ya sasa ya nchi.

“Serikali ikatafakari upya hatua hiyo kwani inarudisha nyuma kama nchi katika hatua ambazo tayari tumeziacha kwa gharama kubwa ya Muda na fedha za watanzania ambazo zingeweza pengine kutumika kwenye shughuli zingine muhimu na za maendeleo,” amesema Henga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles