25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wadaiwa sugu maji kufungiwa mita zinazokata madeni

Na Amina Omari -Tanga

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amewaagiza wakurugenzi wa mamlaka za maji nchini kuanza kufunga mita za malipo ya awali kwa wadaiwa sugu.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya biashara na utalii Mkoa wa Tanga yanayofanyika eneo la Mwahako jijini hapa.

Alisema ili Serikali iweze kukusanya mapato yake vizuri, ni vema wadaiwa sugu waweze kuwekewa huduma hiyo ya malipo ya awali.

“Nimeshatoa maelekezo kwa wakurugenzi wa mamlaka, kama tunataka kuboresha huduma zetu, lazima tuhakikishe tunakusanya mapato kwa watumiaji wote wa huduma yetu,” alisema Aweso.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Tanga (Tanga UWASA), Godfrey Hilly, alisema tayari wameshaanza kutoa huduma hiyo.

Hilly alisema tayari wameanza kusambaza mita za Lumaku kwa taasisi za Serikali ambazo ni wadaiwa sugu.

Alisema tayari huduma hiyo imeweza kuonesha mafanikio makubwa kwani hata yale madeni yameweza kupungua.

“Mita hizo ambazo unalipia huduma ya maji kabla ya kutumia, zina uwezo wa kutoa huduma ya maji na wakati huo huo kupunguza deni la mteja,” alisema Hilly.

Alisema kutokana na gharama kubwa ya uagizaji wa mita hizo, sasa watawafungia wadaiwa sugu pekee ili kupunguza gharama kwa mamlaka hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles