30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wacolombia wapinga makubaliano ya amani

Juan Manuel Santos
Juan Manuel Santos

BOGOTA, COLOMBIA

WAPIGA kura nchini Colombia wameyakataa makubaliano ya kihistoria ya amani kati ya Serikali yao na kundi la waasi wa FARC, matokeo ambayo yamepokelewa kwa mshtuko mkubwa nchini hapa.

Utabiri wa awali uliashiria kuwa kura hiyo ya maoni ingepita kwa kishindo kikubwa ili kubariki makubaliano ambayo yangekomesha vita vya miaka 52.

Vita hiyo imeangamiza maisha ya watu zaidi ya 260,000, na kuwaacha wengine milioni saba bila makazi.

Rais Juan Manuel Santos ameyakubali matokeo hayo, lakini amesema mpango wa kusitisha mapigano utaendelea kutekelezwa, huku akiahidi kuendeleza juhudi za amani hadi siku yake ya mwisho madarakani.

Kwa upande wake, kiongozi wa FARC, Rodrigo Londono amesikitishwa na matokeo hayo na kusisitiza kwamba yeye pia anataka amani.

“Licha ya hayo, kundi letu limejitolea kupatikana kwa amani na kuheshimu mpango wa kuweka chini silaha.

Zaidi ya watu milioni 13 walipiga kura, lakini wanaopinga makubaliano hayo wameshinda kwa kura zisizozidi 60,000.

Baadhi ya wanaounga mkono makubaliano hayo walionekana wakilia kwa huzuni, kusikitishwa na matokeo hayo huku wale walioyapinga wakishangilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles