Wachina mbaroni kwa udanganyifu

0
989

Phnom Penh, CambodiaPolisi nchini Cambodia, wamewakamata raia wa China zaidi ya 200 wanaoshutumiwa kuwadanganya wananchi nchini China kwenye mtandao.

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani ya Wizara ya Kupambana na Ugaidi na Uhalifu wa Kimataifa, Jenerali Y Sok Khy, amesema wanawake 36 ni kati ya raia wa China 235 waliokamatwa Jumatatu katika vijiji vitatu tofauti katika jimbo la Takeo, kusini mwa mji mkuu, Phnom Penh.

Cambodia, imewakamata na kuwapeleka China, raia  1,000 wa China na Taiwan, wanaodaiwa kushiriki katika uhalifu huo tangu 2012.

Makosa yanafanywa kwa kupiga simu au barua pepe kwenye mtandao na kutumia udanganyifu, vitisho na usaliti dhidi ya waathirika.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here