23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WACHINA KORTINI KWA MENO YA TEMBO

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam


 

MENO YA TEMBOSERIKALI imewafikisha mahakamani raia watatu wa China kwa tuhuma za kuongoza mtandao wa uhalifu wa kusafirisha meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 7.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde akishirikiana na Mwanasheria wa Maliasili, Samson Saye, aliwataja washtakiwa kuwa ni wafanyabiashara Xiao Shaodan (30), Liang Hu (31) na dereva Chen Jianlin (35).

Alisema washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kuongoza mtandao wa uhalifu, kosa ambalo wanadaiwa kulitenda  tarehe tofauti kati ya Januari na Novemba, mwaka 2013 jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa washtakiwa hao na wenzao ambao hawapo mahakamani,  kwa pamoja waliongoza mtandao wa uhalifu kwa kuunda na kwa kutenda kwa makusudi kupata, kumiliki na kusafirisha meno ya tembo vipande 1,023 kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar vyenye thamani ya Sh  7,480,125,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi iahirishwe.

Washtakiwa waliomba kuwasilisha malalamiko yao mahakamani, kwamba kesi hiyo ilishawahi kufutwa katika Mahakama Kuu, Mbeya, lakini wanashangaa kuona imefunguliwa kwa stahili nyingine.

Walidai tangu walipokamatwa waliwekwa mahabusu kwa siku 70 katika Kituo cha Polisi cha Kati, Dar es Salaam.

Akijibu hoja hizo, Hakimu Mwijage aliutaka upande wa Jamhuri kuwa makini na haki za watu na alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu kwa kutajwa. Washtakiwa walirudishwa rumande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles