24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Wachimbaji wampongeza JPM

SEIF TAKAZA – Iramba

WACHIMBAJI wadogo wa madini wa mgodi Sekenke One uliopo Kijiji cha Nkonkilangi wilayani Iramba mkoani wa Singida, wamempongeza Rais Dk. John Magufuli  kwa kuwafungulia soko la kuuza madini ya   dhahabu ambalo limekuwa mkombozi wa kukuza uchumi wao.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti walipotembelea mgodi huo  jana,  Katibu wa Idara ya Ukaguzi  wa mgodi huo, Jackson Masanja alisema wachimbaji wadogo wamefarijika kwa uamuzi wa Rais Magufuli kuanzisha masoko ya  madini jambo ambalo limesaidia  wachimbaji wadogo.

Kupata fedha ambapo nyakati za nyuma walikuwa wakidhulumiwa na walanguzi kwa kulipwa fedha ndogo ambazo zilikuwa hazikidhi mahitaji yao ya msingi.

‘’ Ngugu zangu waandishi wa habari, hatuna budi kumshukuru rais wetu kwa kusikia kilio chetu wachimbaji wadogo kwa kutuanzishia masoko ya kuuza dhahabu kwa bei ilekezi, hii imetufanya sisi wachimbaji wadogo kutembea kifua mbele kwani hadi sasa wengi wetu tumejenga nyumba nzuri , tunasomesha watoto wetu kwa kutumia fedha za madini tukilinganisha siku za nyuma ambapo tulikuwa tukidhulumiwa haki zetu .’’ alisema Masanja

Mkurugenzi wa Sekenke One, Ayubu Mrisho aliwaambia waandishi tangu mgodi huo kufungwa na Serikali, umepoteza ajira za vijana wasiopungua 500.

‘’Tangu  shughuli za mgodi huu kufungwa  na Serikali kutokana kuvunjika nguzo za ndani ya mgodi  na kusababisha  na kutitia,  tumeathirika kwa kiasi kikubwa  kiuchumi,  tunaiomba Serikali kutufungulia ili tuanze uzalishaji, kutozalisha madini si kumetuathiri, hata mapato ya Serikali yameshuka,’’ alisema.

Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachimbaji Wadogo Kisonga Shelui(UWAWAKISHE) Mchongomani, Masumbuko Jumanne alisema awali hawakuwa wanalipa kodi,sasa kila mchimbaji mdogo analipa kodi.

‘’Sasa hivi tunaona manufaa ya kazi ya madini  kwani ofisa madini mkazi Chone Malembo, anatusimamia vizuri hadi sasa kila mmoja wetu  anafaidika na uchimbaji ‘’

‘’Kuhusu suala la ugonjwa wa corona wachimbaji wadogo,   tumepata elimu  kubwa kupitia kwa ofisa madini mkazi, watendaji wa vijiji na kata pamoja na kamati ya usalama ya wilaya yetu jana wamepita kuona kama tunachukua tahadhari ya ugonjwa wa corona’’alisemaMasumbuko.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles