21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

WACHEZAJI WABANWA UDANGANYIFU WA UMRI

NA LULU RINGO


Wachezaji wa mpira wa miguu chini ya miaka 17 na 20 wametakiwa kufikisha taarifa zao sahihi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kufikisha taarifa zao sahihi wanaposajiliwa kwenye vilabu.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto amesema msimu huu shirikisho hilo liko makini kuhakikisha taarifa za mchezaji zinazofikishwa ni sahihi

“Kumekuwa na udanganyifu mwingi sana wakati wa usajili vijana wengi wemekuwa wakidanganya sana hasa eneo la miaka unakuta mchezaji ana umri mkubwa lakini anajishusha ili apate nafasi,” amesema Kizuguto.

Nyaraka wanazotakiwa kuwasilisha wachezaji hao ni pamoja na cheti cha darasa la saba, cheti cha kuzaliwa, cheti cha afya kutoka kwa daktari, makubaliano kati yake na timu husika, historia yake tangu alipokuwa na miaka 12, hati ya kusafiria na majina yanayotumika katika usajili yafanane na yaliyopo kwenye vyeti vyake.

Dirisha la usajili kwa wachezaji chini ya miaka 17 na 20 litafungwa Agosti 17, mwaka na wachezaji wote wametakiwa kukamilisha taratibu zote hadi kufikia tarehe hiyo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles