30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wachezaji wa bei mbaya msimu huu nchini England

John Stones
John Stones

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO

MWISHONI mwa wiki iliyopita dirisha la usajili wa Ligi Kuu nchini England lilifungwa katika kipindi hiki cha kiangazi.

Tayari kila klabu imefanya maamuzi sahihi kutokana na kile ambacho walikuwa wanakihitaji kwa ajili ya msimu huu.

Msimu uliopita klabu ya Leicester City ilifanikiwa kutwaa ubingwa kutokana na ushirikiano ambao aliuonesha kocha wao, Claudio Ranieri pamoja na wachezaji wake.

Ubora wa klabu hiyo ya Leicester City haukutokana na usajili ambao waliufanya kabla ya msimu uliopita kuanza, lakini walifanikiwa kutokana na ubora wao na mshikamano kwa pamoja.

Leo hii SPOTIKIKI inakuletea usajili ambao umefanywa katika kipindi hiki cha majira ya joto kwa kuwachambua wachezaji ambao wamesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha, huku England ikiwa imefunika kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha pauni bilioni 1, tofauti na ligi nyingine duniani.

LEICESTER CITY

Hawa ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, baada ya kuchukua ubingwa huo kuna wachezaji ambao wameondoka na kujiunga na klabu nyingine, lakini kuondoka kwao kukamfanya kocha wa timu hiyo atumie zaidi ya pauni milioni 60 kwa ajili ya wachezaji wapya.

Wachezaji wapya ambao wamesajiliwa katika kipindi hiki na kutajwa gharama zake ni wafuatao:

Islam Sliman, huyu ni mchezaji wa pekee ambaye amesajiliwa na mabingwa hao katika kipindi hiki cha usajili na kutajwa kuwa amesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha ndani ya timu hiyo.

Mchezaji huyo amesajiliwa kwa pauni milioni 29 akitokea klabu ya Sporting ya nchini Ureno, wachezaji wengine wanaofuata kwa kusajiliwa kwa fedha kubwa ni pamoja na Ahamed Musa kwa kitita cha pauni milioni 18 akitokea klabu ya CSKA Moscow.

Wachezaji wengine ni pamoja na Bartosz Kapustka, kwa kitita cha pauni milioni 7, akitokea Cracovia. Mbali na wachezaji hao, kuna wachezaji wengine ambao wamesajiliwa na klabu hiyo lakini kiasi cha usajili wao hakijatajwa.

CHELSEA

Kikosi cha kocha Antonio Conte, klabu ya Chelsea nacho kimefanya usajili kwa ajili ya kujiweka sawa katika kipindi hiki cha usajili.

Mchezaji ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa ndani ya klabu hiyo ni Michy Batschuayi, ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Marseille kwa kitita cha pauni milioni 33.

Mbali na huyo, nyota wengine ambao wamesajiliwa kwa fedha kubwa ni N’Golo Kante ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Leicester City, mchezaji huyo amesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 32.

David Luiz ambaye alikuwa anaitumikia klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, naye amerudi Chelsea, klabu yake ya zamani kwa kitita cha pauni milioni 32, Marcos Alonso, amejiunga kwa kitita cha pauni milioni 23 akitokea Fiorentina.

ARSENAL

Nyota ambao wamesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi hiki ni pamoja na Granit Xhaka, ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Borussia M’gladbach, mchezaji huyo amesajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 35, sawa na Shkodran Mustafi kutoka Valencia kwa pauni milioni 35.

Wachezaji wengine ni pamoja na Lucas Perez aliyetokea klabu ya Deportivo kwa pauni milioni 17, huku Rob Holding aliyetokea Bolton amesajiliwa kwa pauni milioni 2.5. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ametumia zaidi ya pauni milioni 80 msimu huu.

 

BOURNEMOUTH

Kocha wa klabu ya Bournemouth, Eddie Howe, aliamua kukiweka sawa kikosi chake kwa kuongeza wachezaji wenye jumla ya thamani ya pauni milioni 33 ili kuweza kuleta ushindani msimu huu.

Mchezaji ambaye alikuwa wa gharama katika kikosi hicho ni Jordon Ibe, ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Liverpool, mchezaji huyo amejiunga kwa kitita cha pauni milioni 15 na kuwa mchezaji pekee ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa, wachezaji wengine ambao wamesajiliwa kwa fedha nyingi ni pamoja na Brad Smith kutoka Liverpool kwa pauni milioni 6, Lewis Cook kutoka Leeds United kwa kiasi cha pauni milioni 6, wakati huo Lys Mousset akisajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 5.4 akitokea Le Havre.

BURNLEY

Kocha wa klabu ya Burnley, Sean Dyche, ametumia kiasi cha zaidi ya pauni milioni 20 kwa ajili ya kuboresha kikosi chake, mchezaji wa gharama katika kikosi hicho ni Jeff Hendrick akitokea klabu ya Derby County, kwa kitita cha pauni milioni 10.5, huku Steven Defour akitokea Anderlecht kwa pauni milioni 7, wakati huo Johann Berg Gudmundsson akitokea Charlton Athletic kwa pauni milioni 2.5.

CRYSTAL PALACE

Kocha wa klabu ya Crystal Palace, Alan Pardew, ametumia zaidi ya pauni milioni 60 kwa ajili ya kukiweka sawa kikosi chake.

Mchezaji wa bei kubwa katika kikosi hicho ni Christian Benteke kutoka klabu ya Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 32, huku Andros Townsend akitokea Newcastle United kwa pauni milioni 13, James Tomkins, kutoka klabu ya West Ham, amenunuliwa kwa pauni milioni 10, wakati huo Steve Mandanda kutoka klabu ya Marseille, amesajiliwa kwa pauni milioni 1.5.

EVERTON

Kocha wa klabu ya Everton, Ronald Koeman, naye ametumia zaidi ya pauni milioni 61 kwa ajili ya maboresho katika kikosi hicho.

Mchezaji ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa ni Yannick Bolasie kutoka klabu ya Crystal Palace kwa pauni milioni 30, huku Dominic Lewin kutoka Sheffield Unite akijiunga kwa pauni milioni 15, wakati huo Ashley Williams kutoka Swansea City akijiunga kwa pauni milioni 9, Idrissa Gueye kutoka Aston Villa akijiunga kwa pauni milioni 7.1.

HULL CITY

Kocha wa Hull City, Mike Phelan, yeye ametumia kiasi cha pauni milioni 11 kwa ajili ya kuweka kikosi chake katika ubora msimu huu.

Mchezaji ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa ni Ryan Mason kutoka Tottenham, kwa kitita cha pauni milioni 10, huku Will Keane kutoka Man United kwa pauni milioni.1, hata hivyo kuna wachezaji wengine ambao wamesajiliwa lakini kiasi chao hakijawekwa wazi.

LIVERPOOL

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ametumia zaidi ya pauni milioni 64 kwa kuongeza nguvu kwa majogoo hao wa jiji la London.

Wachezaji ambao wamesajiliwa kwa fedha nyingi ni Sadio Mane kutoka klabu ya Southampton, kwa pauni milioni 30, huku Georginio Wijnaldum akitokea Newcastle kwa pauni milioni 25, Ragnar Klavan akitokea Augsburg kwa pauni milioni.5, huku Loris Karius akitokea Mainz kwa pauni milioni 4.

MANCHESTER CITY

Kocha mpya wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ametumia zaidi ya pauni milioni 172 katika kipindi hiki cha usajili.

Mchezaji ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa ni beki kutoka Everton, John Stones kwa pauni milioni 47, Leroy Sane akitokea Schalke kwa pauni milioni 42, huku Gabriel Jesus kutoka Palmeiras kwa pauni milioni 27, Ilkay Gundogan kutoka Dortmund kwa pauni milioni 21, Claudio Bravo kutoka Barcelona, kwa pauni milioni 17, Nolito kutoka Celta Vigo kwa pauni milioni 14 pamoja na Marlos Moreno kutoka Atletico Nacional kwa pauni milioni 4.

MANCHESTER UNITED

Kocha Jose Mourinho inaonekana ametumia fedha nyingi katika usajili wake, ambapo inadaiwa ni zaidi ya pauni milioni 156, huku mchezaji ambaye amesajiliwa kwa fedha nyingi ni Paul Pogba kutoka Juventus kwa kitita cha pauni milioni 89, huku Eric Bailly wa Villarreal akisajiliwa kwa pauni milioni 30, wakati huo Henrikh Mkhitaryan kutoka Dortmund kwa pauni milioni 26.

MIDDLESBROUGH

Imetumia kiasi cha pauni milioni 18 kwa ajili ya kuweka kikosi hicho bora, mchezaji ambaye amesajiliwa kwa fedha nyingi ni Marten De Roon akitokea Atalanta, kwa pauni milioni 12, Viktor Fischer kutoka Ajax, kwa pauni milioni 3 sawa na Antonio Barragan kutoka Valencia.

SOUTHAMPTON

Klabu hiyo imetumia zaidi ya pauni milioni 39 katika kusajili, mchezaji ambaye amesajiliwa kwa fedha nyingi ni Sofiane Boufal kutoka klabu ya Lille kwa pauni milioni 16, Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Bayern Munich kwa pauni milioni 12, huku Nathan Redmond kutoka Norwich City kwa pauni milioni 11.

STOKE CITY

Kikosi hicho kimetumia zaidi ya pauni milioni 9 kwa kuongeza nguvu, mchezaji ambaye amesajiliwa kwa fedha nyingi ni Ramadan Sobhi kutoka Al Ahly kwa pauni milioni 5, huku Joe Allen kutoka Liverpool kwa pauni milioni 3.

SUNDERLAND

Kikosi cha kocha David Moyes, kimefanya usajili wa zaidi ya pauni milioni 26, huku mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha nyingi ni Didier Ndong kutoka Lorient kwa pauni milioni 13, Papy Djilobodji kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8.

SWANSEA CITY

Kwa upande wa klabu hii, aliyeongoza kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi ni Borja Baston kutoka Atletico kwa pauni milioni 15).

TOTTENHAM HOTSPUR 

Aliyesajiliwa kwa fedha nyingi ni Moussa Sissoko kutoka Newcastle kwa pauni milioni 30.

WATFORD

Mchezaji aliyesajiliwa kwa fedha nyingi ni Roberto Pereyra kutoka Juventus kwa pauni milioni 13, huku West Bromwich ni Nacer Chadli kutoka Tottenham kwa pauni milioni 13, West Ham, Andre Ayew, akitokea Swansea City kwa pauni milioni 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles