29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Wachezaji Simba wacharuka

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WACHEZAJI wa Simba wameonekana kujituma zaidi katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam,  kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba wanakabiliwa na mchezo dhidi Ruvu Shooting utakaochezwa Novemba 24, mwaka huu,kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa mwisho uliochezwa kwenye uwania huo, Simba ilitoka suluhu na Tanzania Prisons.

Katika mazoezi ya jana wachezaji wa timu hiyo walionekana kuwa makini kupokea maelekezo kutoka kwa kocha Patrick Aussems kuhakikisha wanaelewa wanachofundisha, lakini kuwa fiti zaidi kabla ya kukutana na Ruvu Shooting ili waweze kushinda.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Aussems alisema anahitaji timu yenye ushindani mkubwa na kuweza kufanya vizuri kwa kila mechi.

“Naendelea na programu ya mazoezi kwa wachezaji ambao hawajaenda timu za taifa na kila mmoja wao anaonesha kujituma na kupambana hivyo ndivyo ninayohitaji kwa kuwa tuna mechi ngumu,” alisema.

Alisema kila timu inaonesha ushindani mkali hivyo ni lazima na wenyewe wapambane bila kuangalia ukubwa au ndogo wa timu ili kupata matokeo mazuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles