26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

WACHAMBUZI WAMBEBA KANTE TUZO YA MCHEZAJI BORA ENGLAND

MARTIN MAZUGWA NA MITANDAO


LIGI Kuu ya England inaendelea kushika kasi huku nyota wanaokipiga katika ligi hiyo wakichuana kuhakikisha wananyakua tuzo mwisho wa msimu.

Kati ya tuzo inayotolewa macho zaidi ni ile ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA), mchezaji bora wa mwaka ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na Riyaz Mahrez raia wa Algeria.

Kumekuwa na mjadala mrefu kwa wachambuzi kuhusu nani anafaa kuchukua tuzo hii msimu huu ambapo kuna majina mengi yamependekezwa lakini ndani ya hayo kuna ambayo yanatajwa mara kwa mara.

Wafuatao ni wachambuzi ambao wametoa orodha ya nyota ambao huenda wakatwaa tuzo hii msimu huu.

Alan Shearer, Danny Murphy, Phil Neville, Pat Nevin, Rachel Brown-Finnis, Mark Schwarzer, Jason Roberts, Dion Dublin, Chris Sutton, Ruud Gullit, Mark Lawrenson, Chris Waddle pamoja na Trevor Sinclair.

Alan Shearer: N’Golo Kante

Orodha ya Shearer

Dele Alli (Tottenham), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Alexis Sanchez (Arsenal).

Nyota huyu wa zamani wa kikosi cha timu ya Taifa ya England na klabu za Blackburn Rovers na Newcastle ni shabiki mkubwa wa kiungo Mfaransa, N'Golo Kante, anayekipiga katika klabu ya Chelsea.

Shearer: Mtu pekee ambaye ataenda kushinda tuzo hii msimu huu ni Mfaransa huyo, namwamini na kumheshimu, anafaa kuichukua, ana kila kitu hakuna wa kumzuia kubeba tuzo hii.

Danny Murphy: Eden Hazard

Orodha ya Murphy

Dele Alli (Tottenham), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), Harry Kane (Tottenham),

N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton).

“Kante hahitaji kusimuliwa amesajiliwa kwa mkataba wa fedha nyingi na anacheza katika timu kubwa lakini hiyo haikumfanya atetereke.

“Sababu moja ya kumweka Eden Hazard na Kante, kuna kipindi unahitaji kitu cha ziada ilikupata kitu bora,” anasema.

Phil Neville: Zlatan Ibrahimovic

Orodha ya Neville

Dele Alli (Tottenham), Diego Costa (Chelsea), Eden Hazard (Chelsea),    Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), N'Golo Kante (Chelsea), David Silva (Man City).

Neville: Zlatan Ibrahimovic ni mchezaji wa daraja la juu duniani. Amekuwa akiibeba United katika kipindi kigumu na inapokuwa ikihitaji matokeo anafaa kubeba tuzo hii.

Angalia jinsi alivyokuwa akibezwa kutokana na umri wake mkubwa lakini haikumfanya akate tamaa jambo lililofanya apate namba ya kudumu kikosi cha kwanza,” anasema.

Pat Nevin: N’Golo Kante

 Orodha ya Nevin

Dele Alli (Tottenham), Christian Eriksen (Tottenham), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Gylfi Sigurdsson (Swansea).

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea, Everton, Tranmere Rovers, Pat Nevin amempa nafasi pia  Kante kutokana na uwezo anaouonyesha msimu huu.

"Kante anaenda kushinda tuzo hii hilo halina ubishi, lakini pia mshambuliaji wa Tottenham, Christian Eriksen, nampa nafasi ni kati ya nyota bora msimu huu pia.

"Watu wengi wanawaangalia zaidi Dele Alli pamoja na Harry Kane katika kikosi cha Spurs, lakini mimi namwangalia zaidi Eriksen, ambaye ni kati ya nyota bora zaidi yao,” anasema.

Mark Schwarzer: N'Golo Kante

Orodha ya Schwarzer

Dele Alli (Tottenham), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), Harry Kane (Tottenham),

N'Golo Kante (Chelsea), David Luiz (Chelsea).

“Kuwa katika klabu ya Chelsea ni hatua kubwa kitendo cha kutoka Leicester City na kuwa katika kiwango kile kile si jambo dogo, kila anapocheza vizuri, Chelsea hucheza vizuri pia na hupata matokeo mazuri,” anasema.

Anafaa kuchukua tuzo hii ameonyesha ukomavu mkubwa tangu msimu uliopita.

Jason Roberts: N'Golo Kante

Orodha Roberts

Dele Alli (Tottenham), Jermain Defoe (Sunderland), Eden Hazard (Chelsea), N'Golo Kante (Chelsea), David Luiz (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton).

Roberts: Kuna mambo mengi yanakuja kutoka kwa Dele Alli, lakini nini unajua kutoka kwa kijana huyo ni mmoja kati ya vijana wenye vipaji vya hali ya juu akiwa na morali ya hali ya juu.”

Lakini kura yangu inaenda kwa Kante. Ni moja kati ya viungo bora wa uzuiaji nchini England pia akiwa na uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi.

Dion Dublin: Jermain Defoe

Orodha ya Dublin

Jermain Defoe (Sunderland), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), Harry Kane (Tottenham), N'Golo Kante (Chelsea),

Michael Keane (Burnley), Romelu Lukaku (Everton).

Dublin: Michael Keane ni kati ya walinzi bora hivi sasa na anafaa kuwa kiongozi uwanjani kutokana na ubora wake.

Lakini Defoe ni mashine ya mabao. Anafunga atakavyo na hivi sasa ni yeye ambaye ameamua kuibeba Sunderland begani.

Moyo wangu unasema Defoe anapaswa kuwa mchezaji bora wa mwaka lakini kichwa changu kinasema mfungaji bora ndiye anapaswa kubeba tuzo hii.

Mark Lawrenson: N'Golo Kante

Orodha ya Lawrenson

Dele Alli (Tottenham), Diego Costa (Chelsea), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton).

Lawro: "Kante, Hazard pamoja na Costa wameongeza utofauti katika kikosi cha Chelsea msimu huu na ndiyo sababu iliyofanya wapande juu ya msimamo.

"Kila mtu anajua kumsajili Kante ni sawa na kusajili wachezaji wawili na pindi anapokuwa majeruhi au anapokumbwa na adhabu huenda kukawa na mtikisiko katika kikosi cha kwanza,” anasema.

Ruud Gullit: Eden Hazard

Orodha ya Gullit

Dele Alli (Tottenham), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd),   Harry Kane (Tottenham),

N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton).

Gullit: Hazard atapata kura yangu, sababu ni mchezaji mzuri na muhimu katika kikosi cha Chelsea ambacho amekuwa akijitoa sana.

 Kante anachukua nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza sikatai, lakini kama ningekuwa kocha wao na ningepewa machaguo ningemchagua Hazard.

John Hartson: N'Golo Kante

Orodha ya Hartson

Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), Harry Kane (Tottenham), N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Alexis Sanchez (Arsenal).

Hartson: Mimi ni shabiki mkubwa wa Alexis Sanchez, ambaye hufunga mabao mazuri na yakuvutia kuyatazama anapokuwa uwanjani.

Nahisi mshindi huenda akawa Hazard au Kante, lakini tuzo hii naamini inaenda kwa Kante, ni mchezaji bora ambaye amevaa vyema viatu vya Claude Makelele," anasema.

Chris Waddle: Eden Hazard

Orodha ya Waddle

Dele Alli (Tottenham), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), David Luiz (Chelsea), Harry Kane (Tottenham), N'Golo Kante (Chelsea).

Waddle: Kante ni mchezaji mzuri na hatari lakini si mchezaji anayevutia kumwangalia pindi anapokuwa na mpira.

Jambo gumu katika mchezo ni kutengeneza nafasi, kufunga pamoja na kuburudisha na vyote hivyo vinaweza kufanywa na mtu mmoja naye ni Edin Hazard.

Sioni mtu wa kumzuia staa huyo wa Chelsea katika kinyang’anyiro cha msimu huu,” anasema.

Trevor Sinclair: N'Golo Kante

Orodha ya Sinclair

Dele Alli (Tottenham), Gary Cahill (Chelsea), Eden Hazard (Chelsea), N'Golo Kante (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Gylfi Sigurdsson (Swansea).

Sinclair: Gary Cahill ni nahodha mzuri na kiongozi bora anapokuwa uwanjani.

Amekuwa akibadilika kila msimu tangu alipokuwa Aston Villa kisha Bolton viatu vya nahodha John Terry vinamtosha anafaa kuwa kiongozi.

Lakini Kante ni kiungo aliyekamilika, ana kila kitu ni mpambanaji na mzalishaji yupo kama kiwanda.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles