26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunifu zaidi ya 40 kukutana kwenye Jukwaa la Swahili Fashion Week Dar

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

WABUNINI zaidi ya 40 ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kuonyesha mavazi katika Jukwaa la Swahili Fashion Week, mwaishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa At Parthenon jijini Dar es Salaam.

Huu ni msimu wa 15 wa jukwaa la Swahili Fashion Week, ambalo limekuwa frusa kwa wabunifu, wanamitindo na wadau wa tasnia ya mitindo kwa kutoa nafasi ya kuonyesha kazi zao na kuwakutanisha wanatasnia kwa lengo la kutanua wigo wa biashara ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na wandishi wa habari muasisi wa jukwaa hilo, Bunifu mkongwe hapa nchini Mustapha Hasanali, amesema wana furaha kubwa haikuwa safari rahisi kufikia miaka 15 katika tasnia ikiwa ndio jukwaa kubwa Afrika Mashariki.

“Haikuwa rahisi kufika hapa leo tulianza na wabunifu sita idadi ya wabunifu ilizidi kuongezeka mpaka leo hii tunao 40 kikubwa zaidi jukwaa letu ndio jukwaa kubwa katika ukanda huu ndio sababu wengi waliofanikiwa kushiriki biashara zao zimeendelea,” amesema Hasanali.

Mbali ya kuonyesha mavazi kutakuwa na utolewaji wa tuzo zaidi ya 26 kwa wabunifu, wanamitindo na wadau ambao wamefanya vizuri katika tasnia ya mitindo kwa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles