24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunifu kufuatwa vijijini

Asha Bani, Dar es Salaam

Serikali imeagiza wabunifu mbalimbali nchini kufuatwa maeneo ya vijijini ili waweze kuonesha kazi zao kutumika na kuleta manufaa kwa taifa.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Julai 2, na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi, William Ole Nasha alipokuwa katika banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo amewataka  kuongeza nguvu ya kuwafuata wabunifu waliopo maeneo ya vijijini na kuwasaidia kuonekana kwa kazi zao.

“Nimetembelea mabanda takribani nane yaliyokuwa chini ya wizara hii lakini nimeona kuna wabunifu wengi wapo na wanabuni kazi mbalimbali zenye uwezo mkubwa wa kusaidia taifa hili hivyo ni vyema wakafuatwa katika maeneo yao na Costech mkawa katika mstari wa mbele kuwasaidia wabunifu hao.

“Mfano nikiwa katika banda la Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) nimeona wabunifu wa mitambo ya umeme unaosaidia katika masuala mbalimbali ya kiusalama hii itasaidia mkaweza hata kuwapa mitaji wakafanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na mashirika makubwa kama Shirika la Umeme nchini (Tanesco),” amesema.

Katika banda la VETA kuna mbunifu amefanikiwa kutengeneza mfumo unaopiga simu wenye kama eneo la nyumba lina hatari ikiwamo gari au lifti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles