23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wabunifu 30 kuchuana Stara Fashion Week

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

WABUNIFU wa mavazi 30 wanatarajiwa kuchuana vikali katika jukwaa moja la Stara Fashion Week, kwa kuonyesha kazi zao kuanzia June 1 hadi 2 katika ukumbi Le Maraheb Masaki jijin Dar es Salaam.

Huu ni msimu wa nne wa tamasha hili ambao utakutanisha wabunifu kutoka sehemu mbalimbli ndani ya nchi na nje ya Tanzania kuonyeshaa umahiri wao katika mavazi yenye stara.

Akizungumza na Mtanzania Digital Juni 30, 2022 moja ya waasisi wa tamasha hilo, Asma Makau, amesema jukwaa hilo ni mahususi kwa kuonyesha nguo zenye kujistri na kutoa frusa kwa wabunifu kujitangaza.

“Hii ni frusa kwa wabunifu wetu wa Afrika kuonyesha kazi zao ambazo zimekuwa na wadau wengi kutokana na tamasha hili pia imekuwa ni sehemu ya kuwakutanisha wabunifu na wateja pamoja na kutanua wigo kwa kukutana na wabunifu wakubwa kutoka nje ya Tanzania,” anasema Makau.

Ameongeza kuwa mwaka huu kuna wabunifu 30 ambao 15 wataonyesha siku ya kwanza na 15 watafunga siku ya pili ambayo ita ambatana na utoaji tuzo kwa wadau, wabunifu na wanamitindo katika vipengele tofauti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles