25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WATENGEWA CHUMBA MAALUMU CHA KUNYONYESHA WATOTO

NA KULWA MZEE-DODOMA

BUNGE kwa mara ya kwanza limetenga chumba maalumu cha kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga.

Tangazo hilo lilitolewa jana na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya maswali na majibu.

“Waheshimiwa wabunge, chumba kwa ajili ya watoto kimetengwa katika jengo la zamani, Jengo la Pius Msekwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Ulinzi wa Bunge.

“Bunge limetenga chumba maalumu kwa ajili ya kunyonyesha kwa wale wabunge wenye watoto wachanga.

“Kuanzia sasa mbunge yeyote yule anaweza kuja na mtoto wake na akamnyonyesha kwenye chumba hicho, kisha akaendelea na shughuli zingine za kibunge,” alisema Dk. Tulia.

Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, ilitangaza kuwa wanawake wenye watoto wachanga wanatakiwa kuwanyonyesha kwa kipindi kisichozidi miaka miwili.

Kauli ya Dk. Tulia inashabihiana na semina iliyowahi kutolewa na Spika mstaafu, Anne Makinda kwa kuwataka wabunge wanawake kuwa huru pale wanapotaka kupata wenza wao.

Makinda aliwaambia wabunge wanawake kuwa kitendo cha kuwa mbunge si sababu ya kutopata mtu ambaye unapendana naye katika mahusiano au kukuzuia kupata ujauzito.

Katika semina hiyo ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa Msekwa, Makinda aliwataka wabunge wanawake kujitambua na kuona kuwa wanatakiwa kuwa na haki sawa na wanawake wengine, ikiwa ni pamoja na kubeba mimba bila kuwa na woga.

Kwa sasa wabunge wanawake wameweza kupata mimba wakiwa bungeni bila kuwa na hofu kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wa wabunge wanawake wenye watoto, walisema kuwa chumba ambacho wametengewa na Spika kinatakiwa kuwa na mazingira rafiki ya kunyonyeshea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles