23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WATATU CHADEMA WAACHIWA HURU

Wakili wa Chadema, Peter Kibatala (katikati) akifurahi na wabunge, viongozi wengine wa chama hicho, katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana baada ya kushinda kesi iliyokuwa inawakabili ya kumjeruhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando.PICHA: JOHN DANDE

 

 

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wenzao watatu, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando wameachiwa huru.

Wabunge hao wote wa Chadema, waliokuwa wakidaiwa kumjeruhi Mmbando wakati wa uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, waliachiwa huru jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Mahakama iliamua kuwaachia huru, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka na kuwaona washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Shaidi, alisema mahakama iliwaachia huru kwa sababu hati mashtaka iliyopo haiendani na ushahidi unaotolewa.

 Alisema katika ushahidi anayedaiwa kupigwa, Mmbando alidai hakumbuki nani aliyemjeruhi na alipokuwa akiwaelezea washtakiwa alidai walikuwa wakimpokonya nyaraka zilizokuwa zikihusiana na uchaguzi huo.

“Mmbando alidai kashikwa matiti, lakini hajui alishikwa na nani, kielelezo kilichotakiwa kuwasilishwa mahakamani ni PF 3, lakini baada ya tukio alikwenda kujitibia nyumbani kwa kumeza panadol,”alisema hakimu Shaidi.

Walioachiwa huru, ni Kubenea, Mdee, Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema , mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu.

 Kesi hiyo, ilikuwa ikiendeshwa na Wakili wa Serikali, Flontina Sumawe  ambaye aliita mashahidi watatu kutoa ushahidi upande wa mashtaka ambapo Machi 14,mwaka huu walifunga ushahidi.

Awali  walikuwa wanadaiwa Februari 27,mwaka jana, katika ukumbi wa Karimjee Wilaya ya Ilala,Dar es Salaam walifanya kosa la kumjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha wakati wa uchaguzi wa meya na naibu meya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles