24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wataka wanne tu wakigeni waanze Ligi Kuu

Ramadhan Hassan -Dodoma

WABUNGE wametaka wachezaji wa kulipwa wanaonza kikosi cha kwanza kutozidi wanne, ili kuwapa nafasi wachezaji wazawa.

Wakichangia jana bungeni bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa mwaka 2020-2021,wabunge hao walidai kwamba wachezaji wa kulipwa wanaotoka nje ya nchi wamekuwa wengi hivyo kuna haja ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuliangalia kwa umakini jambo hilo.

Mbunge wa Kilolo,Venance Mwamoto(CCM), alisema TFF inatakiwa kuweka utaratibu wachezaji wa kulipwa wanaonza kikosi cha kwanza kutozidi wanne ili kuwapa nafasi wachezaji wazawa.

“Wachezaji wanatoka nje ya Tanzania kwa sasa wapo wengi lakini suala la wanaotakiwa kuanza katika kikosi cha kwanza ni vizuri ukawekwa utaratibu mzuri zaidi na mimi nashauri wawe wasizidi wanne,”alisema.

Alitolea mfano wa timu ya Taifa ya Uingereza kwa kusemna kutofanya kwake vizuri katika michuano mbalimbali kutokana ligi za nchi hiyo kujaza wachezaji wengi wa kulipwa hivyo ni vizuri TFF ikaliangalia jambo hilo.

Mwamoto pia aliishauriTFF kurudisha mashindano ya Taifa akisema wakati yanafanyika yaliibua vipaji vya wachezaji wengi.

“TFF waje kwetu wabunge tuwape maoni jinsi ya kuendesha soka la Tanzania,”alisema Mwamoto.

Mbunge wa Mufinga Mjini, Cosato Chumi (CCM), alisema malalamiko ya waamuzi kuchezesha chini ya kiwango yamekuwa mengi hivyo kuna haja ya TFF kuliangalia jambo hilo kwa umakini.

“Bila kuwa na waamuzi bora hatuwezi kuwa na ligi bora hivyo jambo hili tunaomba liangaliwe kwa umakini,”alisema Chumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles