24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wataka Serikali iangalia hatima ya walimu shule binafsi

Ramadhan Hassan -Dodoma

BAJETI ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ya zaidi ya Sh trilioni 1.3 kwa mwaka 2020/21, imepitishwa mwishoni mwa wiki  bungeni jijini Dodoma, huku baadhi ya wabunge wakishauri mambo kadhaa, ikiwemo yaangaliwe  hatma ya baadhi ya  walimu wa shule binafsi kutokana na janga la corona,ujenzi wa maabara,ubora wa elimu,utoaji wa mikopo katika elimu ya juu.

Wakichangia mjadala wa bajaeti hiyo,mwishoni mwa wiki wabunge wengi  walihoji zaidi kuhusiana na suala la umaliziaji wa baadhi ya majengo ya maabara ambayo wananchi wengi wamejitolea kujenga huku Serikali ikiwa kimya kuyamalizia.

Mbunge wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe (CCM), alisema  ujenzi wa maabara umetekelezwa kwa asilimia 30 nchini, huku asilimia 70 ukiwa bado.

Aliiomba wizara kuangalia  jinsi ya kumalizia maabara hizo.

“Tuhakikishe tunazijengea  shule zetu zote maabara, tumepita miaka 10 wanawanchi wanajenga, nataka niwapongeze kwa sababu shule zetu zimejengewa kwa asilimia 30 na 70 bado,tumefika wakati lazima tukamilishe kwa wakati hili ni muhimu zaidi,”alisema.

Alionesha kushangazwa na wale wanaotaka masomo yote yafundishishwe kwa lugha ya Kiswahili. Alidai mfano somo la Hisabati wanafunzi wanafundishwa kwa lugha hiyo, i wanaofaulu ni asilimia 17 pekee.

“Watu wengi wanaamini umefika wakati tufundishe kwa Kiswahili kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu ,hawajaangalia hesabu inavyofundishwa,darasa  la kwanza hadi la saba inafundishwa kwa  Kiswahili, ni asilimia 17 tu ndiyo wanafaulu,”alisema

Alishauri ili ubora wa elimu uweze kuwa juu, lazima Serikali iboreshe mfumo wa elimu kwa kuwajengea uwezo walimu wa masomo husika.

Kuhusiana na suala la mikopo ya elimu ya juu,Dk.Maghembe alisema lazima jambo hilo liangaliwe kwa umakini kwani wanaokosa mikopo wengi ni  watoto wa maskini.

Mbunge wa Muleba Kaskazini,Charles Mwijage (CCM) alisema kuna haja ya Serikali kujenga mabweni mengi ili kuwasaidia watoto wa kike wasipate mimba.

“Hata wasichana tuwafungie shule wale ambao wameolewa achana nao tuwajengee mabweni ili wasipate mimba ,Serikali nendeni mkakope wamama wasome wote.

“Lazima Serikali iwekeze katika elimu, walimu wapewe uwezo mkubwa ili tuweze kwenda huko katika viwanda,”alisema

Kuhusu walimu wa shule binafsi,Mwijage alisema jukumu la kutoa elimu ni la Serikali, kuna haja ya kuangalia pia jinsi ya kuwasaidia walimu wa shule binafsi.

“Naiomba Serikali wale wafanyakazi muwapatie kiasi fulani cha fedha, sisi Tanzania fedha tunazo kama hatuna tukakope benki, muwape, watu binafsi wametuokoa hawa wanalea watoto wetu, Serikali nenda kamchukue mtoto wako analala njaa ambaye ni huyu mwalimu.

“Tusipowasaidia mfumo mzima utakuwa umeteketea,tutaanza kwenda Kongo (DRC)   mtoto wako anatoka huko, badala ya kukusaidia anacheza ndombolo,”alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu,Benardetha Mushashu (CCM) aliiomba wizara kutoa maneno ya faraja kwa wanafunzi ambao kwa sasa wapo nyumbani.

Alisema wanafunzi wa madarasa ya mitihani wapo katika kipindi kigumu hivyo kuna haja ya Wazara kila wiki kutoa maneno ya faraja kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles