30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WABUNGE WAMPINGA TRUMP KUPUNGUZA MISAADA YA KIGENI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump kwa mara ya kwanza amelihutubia Bunge la Marekani katika hotuba iliyopingwa na baadhi ya wanachama wa Chama chake cha Republican hasa mpango wake wa kupunguza misaada ya kigeni.

Ni hotuba iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa hadi pale Rais Trump aliposimama mbele ya Bunge na kulihutubia.

Hata hivyo, hotuba yake iliegemea zaidi masuala ya uhamiaji na kuwapunguzia kodi wananchi bila kugusia soko la fedha kama ilivyotarajiwa na wawekezaji na wafanyabiashara.

Lakini pia alionyesha kidogo kulegeza msimamo wake juu ya wahamiaji haramu, akisema licha ya mageuzi, wale wenye vipaji na ujuzi mkubwa wanakaribishwa Marekani.

Lakini baadhi ya wajumbe wa Republican wanapinga hatua anazotaka kuzichukua, ikiwamo kupunguza kiwango kikubwa cha misaada ya Marekani kwa nchi za kigeni.

Kiongozi wa Seneti, Mitch McConnell ambaye aliwahi kuongoza jopo lililosimamia bajeti ya misaada ya nje, amesema haungi mkono kupunguza misaada ya nje. 

Rais Trump katika mpango wake analenga kupunguza misaada hiyo na badala yake kuiongezea Wizara ya Ulinzi kiasi cha dola bilioni 54.

Hatua hiyo itapunguza kwa asilimia 37 fedha kutoka Wizara za Mambo ya Ndani na ile ya Diplomasia na Mambo ya Nje.

Punguzo hilo bila shaka litaleta ugumu usiofichika katika wizara hizo.

Mkurugenzi wa Masuala ya Bajeti wa Ikulu, Mick Mulvaney, amesema anachotaka kufanya Rais Trump ni kupunguza matumizi ya nje na badala yake kuzirejesha fedha hizo kwa matumizi ya ndani.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles