28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wampa kibarua Waziri Lwenge

lwengeNA HADIA KHAMIS, DAR  ES  SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge  ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dk. Mary Nagu amemwagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Grayson Lwenge, kushirikiana na mamlaka zake za maji kuwadhibiti mawakala wa maji ili waache tabia ya kutoa huduma hiyo kwa wananchi kwa gharama kubwa.

Alisema baadhi ya mawakala hao, ni wajanja wamekuwa wakijipatia fedha nyingi kwa kuwauzia wananchi maji kwa bei kubwa jambo ambalo linafanya waichukie Serikali yao.

“Maji ni uhai, maji ni siasa na maji ni maendeleo. Nakuagiza waziri na timu yako mhakikishe wananchi wanapata majisafi na salama tena kwa gharama nafuu.

“Ujanjaujanja unaofanywa na baadhi ya mawakala wa maji, lazima udhibitiwe haraka, hakikisheni miundombinu, vyanzo na mito vinalindwa kikamilifu,” alisema.

Nagu  alilitoa agizo  hilo mwishoni mwa wiki, wakati kamati yake ilipotembelea mradi wa kusambaza mabomba kutoka Ruvu Chini kwenda Dar es Salaam.

Alisema kamati yake imeridhishwa na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ruvu Chini hadi katika matanki ya kuhifadhia maji yaliyopo Chuo Kikuu cha Ardhi, ambao sasa umekamilika na kuanza kutoa huduma.

Alisema mradi huo, umesimamiwa vizuri na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), ambayo imefungua milango ya kuwapunguzia kero wananchi.

Mradi huo wenye urefu wa kilomita 56 kutoka Ruvu hadi Dar es Salaam, umegharimu Sh bilioni 141 na  umejengwa na Kampuni ya Sino Hydro ya China.

“Nawapongeza kwa dhati DAWASA kwa kuusimamia kikamilifu mradi huu ambao ni dira ya Serikali yetu.

“Kukamilika kwake kumeonyesha dhamira ya dhati ya Serikali kuwatumikia wananchi wake kwa vitendo kwa kuwapatia majisafi na salama, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya CCM,” alisema Nagu.

Kwa mujibu wa Nagu, kukamilika kwa mradi huo kutawezesha wakazi wa Dar es Salaam na majirani zake kupata ongezeko la maji la lita milioni 270 kwa siku.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Grayson Lwenge alisema wizara yake imejipanga kutoa huduma hiyo bila upendeleo.

“Mradi huu umeanza kazi na mpaka dakika hii baadhi ya mabomba yameanza kupasuka kutokana na kasi ya usukumaji maji kuwa kubwa.

“Kazi iliopo sasa ni kukaratabati miundombinu yetu ili tuweke mabomba mapya na kuondoa yale ya zamani yaliyochoka,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles