29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

WABUNGE WAMGOMEA TRUMP KUPUNGUZA MISAADA AFRIKA

WASHINGTON, MAREKANI


BUNGE la Marekani linatarajia kupiga kura makubaliano yanayounga mkono bajeti itakayobakisha sehemu kubwa ya programu za misaada kwa Afrika na kutoa dola bilioni moja kukabiliana na tishio la njaa.

Makubaliano hayo yalitangazwa jumatatu wiki hii baada ya wabunge kukataa mpango wa kupunguza misaada unaokusudiwa kufanywa na Rais Donald Trump anayetokea Chama cha Republican.

Matokeo hayo yanatokana na kutokuwa tayari kwa wabunge waandamizi wa Republicans kukata fedha za programu hizo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo Marekani (USAid).

Sehemu kubwa ya wabunge wanaomuunga mkono Trump, waliopendekeza kukatwa kwa misaada walijikuta wakikosa nguvu baada ya uamuzi wa viongozi wa Republican kuingia makubaliano na wabunge wa Chama cha Democrat walio wachache kuukataa mpango wa Rais.

Kutokana na uamuzi huo, Rais Trump amepata pigo katika juhudi zake za kuweka ‘Marekani Kwanza’ kwa gharama ya nchi masikini.

Hata hivyo, Rais Trump amesema hana jinsi atakubaliana na mpango wa matumizi ya serikali kuu unaowasilishwa na Bunge.

Makubaliano baina ya Republican-Democratic yanahusu bajeti ya Marekani kwa mwaka wa fedha 2017 unaoishia Septemba 30.

Lakini Trump ameapa kuwa atahakikisha azma yake ya kupunguza fungu kwa Wizara ya Mambo ya Nje na USAid kwa mwaka wa fedha 2018 inatimia.

Waungaji mkono wa misaada ya Marekani kwa Afrika nchini hapa wamesifu makubaliano yaliyofikiwa na vyama vya Republican na Democrat.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles