32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

WABUNGE WALIOSUSA HOTUBA YA RAIS ZAMBIA WASIMAMISHWA

 

 

Lusaka,  Zambia

BUNGE la Zambia limewasimamisha wabunge 48 wa upinzani kwa   siku 30 kwa kususa hotuba ya Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo miezi michache iliyopita.

Spika wa Bunge hilo, Patrick Matibini amesema ametumia mamlaka yake ya sheria kuwasimamisha wabunge 48 wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND), kwa   kutoka nje ya Bunge  Machi mwaka huu  wakati wa hotuba ya Rais Lungu.

Amesema iwapo wabunge hao hawamtambui rais aliyechaguliwa na wananchi kwa njia halali, basi wana hiari ya kujiuzulu.

Wabunge hao wa upinzani walitoka nje wakisema kuwa hawamtambui Rais Lungu kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi wa Agosti mwaka jana.

Matibini amesema wabunge wa UPND hawatalipwa mshahara katika muda huo wa mwezi mmoja wala kuruhusiwa kuingia katika jengo la bunge.

Kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema aliyewania kiti cha urais katika uchaguzi uliopita na kutoa upinzani mkali kwa Rais Lungu, anashtakiwa kwa   uhaini na yupo kizuizini tangu  Aprili mwaka huu.

Mwaka jana katika uchaguzi mkuu uliyofanyika Agosti 11, matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalionyesha kuwa Hichilema alikuwa anaongoza.

Hata hivyo,  matokeo yaliyotangazwa baadaye na Tume ya Uchaguzi yalionyesha   Lungu ndiye aliyekuwa mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 50 ya kura jambo ambalo liliibua mgogoro mkubwa wa siasa unaoendelea nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles