WABUNGE WALIOPATA AJALI WAFIKISHWA MUHIMBILI

0
1014

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Wabunge sita waliopata ajali mkoani Morogoro usikuwa wa kuamkia leo, wamefikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Steven amesema wabunge hao ambao wameumia maeneo ya kichwani, shingo, mikono, miguu na kifua, hali zao zimeanza kuimarika.

“Tumewapokea saa saba mchana huu, katika Kitengo cha Magonjwa ya Dharura, Mbunge wa Makunduchi Haji Amir Haji ambaye hali yake ilielezwa kuwa mbaya ameumia sehemu ya kichwani hivi sasa hajambo, anaendelea kupatiwa matibabu,” amesema.

Amewataja wabunge wengine waliowapokea ni Juma Othman Hija (Tumbatu), Makame Mashaka Foum, Khamis Ali Vuai na Bhagwanji Mangalal Meisuria.

Wabunge hao walipata ajali eneo la Mikese mkoani Morogoro, wakakimbizwa Hospitali ya ya Morogoro kwa matibabu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here