29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WADAI SDG’S HAITEKELEZEKI

                            Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema)

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

WABUNGE wamesema Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hayawezi kutekelezwa kutokana na vipaumbele vilivyowekwa kutozingatia mahitaji ya taifa.

Wakizungumza mjini hapa jana katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), baadhi ya wabunge walisema kuwa malengo hayo hayakuangalia nini kilitakiwa kupangwa kwa wakati huo.

Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema), alisema malengo hayo yangeendana na ongezeko la uchumi wa kilimo, lazima kungekuwa na mabadiliko.

“Lakini suala la kutaja kuongezeka kwa uchumi kwa kutumia makaratasi halina maana kwa malengo endelevu,” alisema.

Pia alisema kwa sasa kilimo kinashuka badala ya kupanda na kuonyesha shaka kubwa kuhusu utekelezaji wake kwa sababu mkazo ungewekwa hali ya umasikini ingepungua kwa asilimia 50.

Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF), alisema malengo 17 yanayotangazwa na Serikali yatapata ugumu wa utekelezaji wake na yatabaki katika vitabu.

Mtulya alisema malengo hayo yalichukuliwa kutoka nchi za kigeni badala ya kuweka mkakati wa kuyapanga kwa kuangalia vipaumbele vyetu jambo ambalo litakuwa gumu kuyatekeleza.

“Katika matamko yanaonekana kuwa mazuri, lakini ukweli ni kwamba yamechukuliwa kutoka nchi nyingine badala ya kuangalia vipaumbele vyetu,” alisema.

Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko (CCM), alisema malengo endelevu yapo kwa kuyainua baadhi ya mataifa, lakini kwa Tanzania itakuwa ni ngumu kuyafikia yote.

“Taifa linakabiliwa na changamoto nyingi zinazopaswa kutatuliwa ili kulifanya lisonge mbele, lakini kwa namna malengo hayo yalivyowekwa, huenda ikawa ni vigumu kuyafikia,’’ alisema.

Akijibu baadhi ya hoja, mmoja wa wawezeshaji katika semina hiyo, Ambrose Mugisha, alisema mipango iliyowekwa katika malengo hayo ni mizuri na inapaswa kusimamiwa kikamilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles