31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

WABUNGE WA UINGEREZA WAKATAA BREXIT BILA YA MAKUBALIANO

Wabunge wa Uingereza wamepitisha pendekezo la kukataa Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya ama Brexit bila ya makubaliano.

Muswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha Labour Yvette Cooper, utamtaka Waziri Mkuu Theresa May kuuomba Umoja wa Ulaya kuongeza muda kwa Uingereza hadi pale itakapopata makubaliano.

Muswada huo ulipitishwa kwa kura 313 dhidi ya 312 bungeni, lakini bado utasubiri kuthibitishwa siku ya Alhamisi.

Kura hiyo inakuja baada ya May kukutana na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn kujaribu kukubaliana kuhusu Brexit na kuondoa mkwamo ulioko bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles