23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge kwenda Misri kuishangilia Taifa Stars

Ramadhan Hassan,Dodoma

Wabunge wametakiwa kwenda Misri kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Akizungumza leo Mei 22 bungeni Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema timu ya Bunge Sc inaendelea  kuratibu zoezi la kujiandikisha wabunge ambao wataenda kushuhudia fainali hizo. 

“Bunge Sc wanaendelea kuratibu utaratibu wa wabunge na tutaenda Misri tukiongozwa na mheshimiwa Waziri Mkuu wakati timu yetu ya Taifa itakapoenda kucheza AFCON,” amesema Ndugai.

“Tuchangie masuala ya nauli ni vyema wabunge tuonesha mfano kwa kujiandikisha kwa wingi na kuwahamasisha wengine na mipango iende haraka kwa sababu Booking za hoteli zitajaa itabidi tufanye mapema, tukijiandikisha mapema naamini itawapa moyo vijana wetu,” amesema Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles