24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Chadema, Meya Ubungo washtakiwa kufanya fujo Gereza la Segerea

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Wabunge watatu wa Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini) na Jesca Kishoa (Viti Maalumu), Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, Patrick Asenga na wenzao wamefikishwa mahakamani kwa mashtaka saba ikiwamo kuharibu lango la Gereza la Segerea na kumchania shati Askari Magereza.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani saa nane mchana leo Jumatatu Machi 23, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Renatus Mkude amedai washtakiwa walitenda makosa hayo Machi 13 mwaka huu katika Gereza la Segerea.


Amedai wshatakiwa hao wanadaiwa walikaidi amri halali ya Sajent John aliyekuwa katika geti la kuingia gerezani, walifanya mkusanyiko usio halali na waliharibu mali.


Inadaiwa kwa pamoja washtakiwa walishirikiana kufanya uharibifu katika geti kuu la kuingia gerezani, geti ni mali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.


Pia mshtakiwa Mdee, Bulaya na Boniface wanashtakiwa kwa kutumia lugha ya kuuzi kwa Sajenti John.


Washtakiwa walikana mashtaka, wamekubaliwa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja, mwenye barua na kitambulisho na atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles