27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

WABUNGE CCM WAENDELEA KUMSIFU RAIS MAGUFULI

                      Rais Dk. John Magufuli

Na Kulwa Mzee -Dodoma

MBUNGE wa Bukene, Suleiman Zedi (CCM), amesema ujasiri na hatua zinazochukuliwa na Rais Dk. John Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi, ubadhirifu na kuzilinda rasilimali za nchi umevuka mipaka ya Tanzania.

Kauli hiyo aliitoa bungeni juzi wakati akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Zedi anayeiwakilisha Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), alisema kila anaposhiriki vikao vya Bunge hilo, wajumbe wenzake wanamuulizia Magufuli.

“Nilipokwenda kwenye vikao vya Bunge la SADC ambalo lina wanachama kutoka nchi 14 za Afrika, kila ninapojitambulisha basi wajumbe wanauliza Magufuli.

“Wajumbe wengi wa Bunge hilo wanahoji hivi Magufuli alikuwa nani kabla ya kuwa rais wa nchi,” alisema.

Kuhusu gesi asilia, aliishauri Wizara ya Nishati na Madini kutafuta ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge lililopita ya Nishati na Madini, ichukue mapendekezo na ushauri wake na wayafanyie kazi.

“Nilikuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ndogo ya Bunge ya Nishati na Madini, hivyo naishauru wizara husika kuitafuta ile ripoti ili ichukue yale mapendekezo yetu kwa sababu ni mazuri na yanaweza kusaidia kwenye sekta ya gesi asilia,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve (CCM), alisema Magufuli ameuthibitishia umma kwamba rasilimali za nchi hazipotei.

Pia aliitaka Serikali kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kumiliki hisa katika kampuni za simu kwa sababu mwitikio wao bado ni mdogo.

Mbunge wa Msimbo, Richard Mbogo (CCM), aliishauri Serikali kuwa na soko la madini ili iweze kukusanya mapato mengi katika sekta hiyo.

Alisema wafanyabiashara wengi wa madini hawasemi ukweli kuhusu mapato wanayopata ili waweze kulipa kodi stahiki, hivyo ni vema kukaanzishwa soko la madini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,673FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles