LONDON, UINGEREZA
WABUNGE 40 wa Chama tawala cha Conservative wamepanga kukwamisha mpango wa Waziri Mkuu Theresa May wa kujiondoa EU.
Kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri anayehusika na masuala ya Brexit, yaani kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Steve Baker wataupiga chini mpango huo iwapo utaifanya Uingereza iwe mguu mmoja ndani na mwingine nje katika umoja huo.
Mbunge huyo ambaye alijiuzulu uwaziri wa Brexit kama hatua ya kupinga mapendekezo ya May yanayotaka Uingereza kuwa na uhusiano fulani na EU.
Badala yake Baker na wenzake wanataka Uingereza iondoke kabisa kutoka Umoja wa Ulaya.
Ikiwa May atafanikiwa kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya atalazimika kulishawishi Bunge la nchi yake kuyaidhinisha na atahitaji kuungwa mkono na idadi fulani ya wabunge