Wabakwa kwa kula nyama ya ng’ombe India

0
1398

ngombeDELHI, INDIA

MWANAMKE mmoja nchini India amesema yeye pamoja na binamu yake mwenye umri wa miaka 14 walibakwa na genge la watu wanne, ambao pia waliwaua jamaa zao wawili kwa tuhuma za kuwa Waislamu waliokula nyama ya ng’ombe.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 alisema wanaume hao walifanya uvamizi huo katika makazi yao yaliyopo wilaya ya Mewat, jimbo la Haryana Kaskazini wiki mbili zilizopita.

“Pamoja na utetezi wetu kuwa hatukula nyama hiyo, walinibaka mimi na binamu yangu, kisha kumuua mjomba na shangazi yangu,” msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alisema.

Waumini wengi wa dini ya Kihindu huwahesabu ng’ombe kuwa watakatifu na kuchinja wanyama hao kumepigwa marufuku katika majimbo mengi likiwemo Haryana.

Kisa hicho kimezua ghadhabu katika jamii ya eneo hilo, kitu kilichochochea washukiwa kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa yanayohusu ubakaji na mauaji.

Mewat, wilaya iliyo na Waislamu, ikiwa umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu wa Delhi, hivi karibuni iliteka vyombo vya habari baada ya afisa wa cheo cha juu, kuwaambia wanahabari kuwa polisi wataanza kukagua chakula cha biriani kuhakikisha kuwa hakina nyama ya ng’ombe.

Ubakaji na uhalifu katika misingi ya kijinsia ni masuala yaliyoangaziwa zaidi nchini India katika miaka ya hivi karibuni tangu kubakwa na kuuawa kwa mwanafunzi kulikofanywa na kundi la watu mjini Delhi mwaka 2012.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here