HABARI njema kwa Barcelona ni kwamba kuna kampuni ya Dubai imejitokeza kulipa madeni yanayoikabili klabu kongwe hiyo ya La Liga.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, kampuni hiyo italipa deni la euro bilioni 1.5, jambo litakalofufua uchumi wa Barca ulioyumba kwa muda sasa.
Hata hivyo, mkwanja huo si kwamba utatolewa bure, bali Barca watatakiwa kulipa miaka 12 ijayo.
Pia, haitakuwa kulipa deni tu, isipokuwa fedha walizopewa zitapaswa kuambatana na riba.