25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa Kitabu cha Language Supportive Pedagogy: Theory, Implementation and Application wapongezwa

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waandishi wa Kitabu cha Language Supportive Pedagogy: Theory, Implementation and Application wamepongezwa kwa kutunga Kitabu kizuri na ambacho kinamsaidia Mwalimu kutumia lugha rahisi,inayoeleweka iliyojaa mifano rahisi, picha na vielelezo kuhakikisha mwanafunzi anaelewa dhana ambayo inafundishwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jana Jijini Dodoma kupitia mtandao wa Zoom, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na kiongozi Mkuu wa Regional Education Learning Initiatives (RELI) Tanzania,Dk. Maryam Ismail amepongeza waandishi wa kitabu kwa kazi nzuri ya kufikisha habari njema za mradi kwa hadhira pana.

Alisema kitabu hicho kimekuja wakati muafaka kwani Nchi kwa sasa ipo katika mchakato wa kupitia sera yetu ya elimu.

“Tunaamini maarifa yaliyomo kitabuni yatachangia sana katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa watu wetu,”amesema

Kwa upande wake, Dk. Angeline Baret akichangia kwa njia ya mtandao wa Zoom kutoka Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza na mtafiti mkuu wa Mradi wa LSTT alieleza kufurahishwa kwake na jinsi mradi ulivyowagusa wadau wengi.

“Nimefurahi kumsikia mwalimu wa sekondari namna alivyoelezea kuhusu LSTT na msaada wake katika kumjenga kama mwalimu anayejiamini na kufanya kazi yake kwa ufanisi. Ninaamini hatutaishia hapa bali tutaendelea kushirikiana na wadau wote na hasa serikali kuinua ubora wa elimu katika shule zetu,”alisema.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhadhiri wa Chuo cha St John, Dk.Shadidu Ndossa alisema mojawapo ya changamoto kubwa ambayo ipo katika ufundishaji ni namna ya kufundisha ili mwanafunzi aweze kuelewa kwa lugha rahisi,inayoeleweka iliyojaa mifano rahisi, picha na vielelezo.

Dkt.Ndossa amesema kutokana ufundishaji kuwa ni changamoto walipata mradi wa Language Saporting Teaching and Text Book (LSTT) ambao ulikuwa na lengo la kumsaidia mwalimu kuweza kufundisha kwa lugha ya kueleweka.

Alisema kwa kupitia mradi huo wameweza kutunga vitabu vitatu vya Chemisty,Biology na Hisabati ambavyo vimekuwa msaada kwa wanafunzi na walimu.

Alisema mradi huo kwa sasa unaelekea mwishoni na walimu nane kutoka katika mradi waliweza kuandika kitabu kutokana na kushiriki katika mradi huo.

“Ni mradi ambao unahimiza mwalimu kutumia lugha au kuona lugha ni sehemu muhimu kuhakikisha wanafunzi wanaelewa hasa katika masomo ya Sayansi.Kwa mfano mimi katika chapter ambayo nimeiandika kama miongoni mwa waandishi niliandika kuelezea vile vitabu ni namna gani..

“Vimesaidia kumuunganisha mwalimu,mwanafunzi pamoja na vitabu kwa sababu kumekuwa na changamoto vitabu vinatumia lugha ngumu ikiwa ni pamoja na mifano ambayo haipo katika mazingira ya wanafunzi na tunatumia maneno magumu na sentensi ngumu.

“Kwa hiyo mradi wetu huu pamoja na mambo mengine unahimiza mwalimu kutumia lugha rahisi lugha inayoeleweka lugha iliyojaa mifano rahisi,lugha iliyojaa picha na vielelezo kuhakikisha mwanafunzi anaelewa dhana ambayo inafundishwa,”amesema Dk.Ndossa ambaye ni sehemu ya wahariri wa kitabu hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles