31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waandamanaji Sudan waitisha tena maandamano

Waandamanaji nchini Sudan wametoa wito wa kufanyika maandamano makubwa, wakisisitiza kuwa jeshi halina nia thabiti ya kukabidhi madaraka kwa raia karibu wiki tatu baada ya kuuondoa madarakani uongozi wa Omar al-Bashir.

Wito  huo  unakuja  wakati  hali  ya  wasi  wasi  ikiongezeka kuhusiana  na  muundo wa  baraza jipya  la  pamoja  kati  ya  raia  na jeshi  litakaloiongoza  nchi  ya Sudan, wakati waandamanaji wakiimarisha  vizuwizi nje ya  makao makuu  ya  jeshi  katika mji mkuu  Khartoum.

Pande  hizo  mbili  zina  mambo  mengi yanayokinzana  kuhusiana  na  wawakilishi  katika  baraza  hilo  jipya ambalo linatarjiwa  kuchukua  nafasi  ya  baraza  la  kijeshi  ambalo lilichukua  madaraka  baada  ya  kuondolewa  madarakani  Omar al-Bashir Aprili 11  baada  ya  maandamano  makubwa  ya  umma kupinga  utawala  wake  wa  miongo  mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles