27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waandamana kupinga AU Sudan Kusini

Salva Kiir
Salva Kiir

JUBA, SUDAN KUSINI

MAMIA ya wafuasi wa Serikali ya Sudan Kusini wameandamana mjini hapa kupinga pendekezo la viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) kutuma kikosi cha ziada cha jeshi la kulinda amani.

AU ilifikia uamuzi huo baada ya kutokea mauaji ya zaidi ya watu 300 wiki iliyopita baada ya majeshi yanayomtii Makamu wa Rais Riek Machar kukabiliana na vikosi vya Rais Salva Kiir.

Rais Kiir amepinga kutumwa kwa mwanajeshi yeyote zaidi ya wale 12,000 wa Umoja wa Mataifa (UN) ambao tayari wako hapa.

Uamuzi wa kutuma kikosi zaidi kulisaidia jeshi la kulinda amani hapa (UNMISS) ambalo katika siku za hivi karibuni limelaumiwa kushindwa kabisa kulinda maisha ya raia.

Viongozi wengine akiwemo Rais wa Uganda Yoweri Museveni pia wamepinga pendekezo la kuwekewa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha Sudan Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles