23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Waamuzi Simba na Yanga hadharani

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba na Young Africans utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Mei 8, 2021 saa 11: 00 jioni.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetoa orodha hiyo ya waamuzi uzi watakaosimamia sheria 17 za mchezo wa soka siku ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga Jumamosi hii.

Simba SC itashuka katika Uwanja wa Mkapa ikiwa ndiyo timu mwenyeji kumkaribisha mtani wake Yanga kwenye mchezo huo wa Mei 8, 2021 ambao huwenda kuweka wazi mbabe ni nani baina ya timu hizo mbili tangu kubadilisha makocha wapya.

Waamuzi wa mchezo huo wa Mei 8, 2021 ni kama ifuatavyo kwa mujibu wa Shirikisho la soka TFF. Mwamuzi wa kati atakuwa Emmanuel Mwandembwa kutokea mkoani Arusha, mwamuzi msaidizi namba moja Frank Komba kutoka Dar es Salaam, mwamuzi msaidizi namba mbili Hamdani Saidi kutokea Mtwara na Mwamuzi wa akiba akiwa ni Ramadhani Kayoko kutokea Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles