23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Waamuriwa kuchimba kisima cha maji kunusuru wananchi na magonjwa

NA FLORENCE SANAWA-MTWARA

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk. Dorothy Gwajima, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Omary Kipanga, kuhakikisha kinachimbwa kisima mbadala kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na wananchi kutumia maji yasiyo salama katika Kata ya Naguruwe.

Alitoa agizo hilo wakati alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya Nanguruwe katika Halmasharui ya Wilaya ya Mtwara, ambacho ujenzi wake unasuasua na kukutana na wananachi waliolalamikia uwepo wa tatizo la maji.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, alisema kisima mbadala kinapaswa kujengwa haraka ili kuwanusuru wananchi na magonjwa ya mlipuko na typhoid.

“Hili eneo lina watu wengi, wakipata mlipuko tutateseka, tutapata shida, Tamisemi na Wizara ya Afya zitahangaika kuja kuokoa janga hilo,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Kipanga, alisema uchimbaji wa visima umekuwa ukitumia teknolojia hali ambayo likitokea tatizo huchukua muda mrefu kulitatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles