Waajiri Arusha watakiwa kulinda wafanyakazi

0
1767

Na Mwandishi Wetu

Waajiri mkoani Arusha wametakiwa kuweka mfumo madhubuti ili kulinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali katika maeneo yao ya kazi .

Wito huo umetolewa leo Novemba 21, jijini Arusha na Katibu Tawala wa mkoa huo, Richard Kwitega alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika ufunguzi wa mafunzo maalumu ya Vision Zero.

Mafunzo hayo ya Vision Zero yanaandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) jijini Arusha, maalamu kwa wamiliki wa meneo ya kazi mkoa wa Arusha.

Kitwenga amesema uwepo wa mifumo mizuri maeneo ya kazi itasidia kuwakinga wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali zinazotokea maeneo ya kazi.

Baadhi ya Wawakilishi wa Viwanda,wafanyabiashara,taasisi,kampuni za  mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini, mafunzo ya Vision zero Mkoani Arusha

Amesema wafanyakazi ni kipuri namba moja, kwa Taasisi au kampuni yoyote katika ufanisi wa kazi yoyote na kwamba mchango wao ni mkubwa..

“Wafanyakazi wana mchango mkubwa sehemu ya kazi hivyo hawana budi kuhakikishiwa usalama wao dhidi ya magojwa na ajali zinazoweza kutokea sehemu za kazi, ilikuwawezesha kufikia malengo waliojiwekea,” amesema Kitwenga.

Aidha, Kitwenga amesisitiza waajiri kutoa ushirikiano kwa OSHA ilikuhakikisha suala hilo linatekelezwa bila vikwazo.

“Wafanyakazi wanamchango mkubwa kwenye suala la usalama na afya mahali pa kazi kwani wao ndio watendaji wa kazi, endapo ushirikiano utakuwepo baina yao, itasaidia kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi.

“Suala hili ni la pande tatu yaani mwajiri,mwajiriwa na serikali na endapo ushirikiano huo utadumishwa basi ajali na magonjwa yatapungua ama kuisha kabisa sehemu za kazi,” amesema Kitwenga.

Amewataka wafanyakazi kujenga utamaduni wakujilinda wao wenyewe wakiwa kazini, kwani wao wanabeba jukumu kubwa la kujilinda dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi kutokana na majukumu yao ya kila siku.

Akiongea kwa niaba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa Usalama na Afya, Mhandisi Alex Ngata amesema kampeni ya Vision Zero ni kampeni ya kidunia nzima ambapo nchi mbalimbali duniani zinatekeleza.

“Hii ni kampeni ya dunia nzima ambapo lengo kuu la Vision zero ni kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi,” amesema Mhandisi Ngata.

Aidha, Mhandisi Ngata amesema uwepo wa mfumo sehemu za kazi utawawezesha waajiri kujikagua wenyewe na hivyo kuweza kuzuia magonjwa na ajali sehemu za kazi.

“Mfanyakazi ni msingi imara katika biashara na uzalishaji ambao OSHA unaungalia bila wao hawawezi kuzalisha na kufanyabiashara hivyo ni muhima kuzingatia usalama na afya zao, wakiwa kazini ni vema kuwepo na mfumo maeneo yenu ya kazi ilimuweze kulinda nguvu kazi hiyo,” amesema Mhandisi Ngata.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema, Vision zero itawasaidia kwenda kuweka mifumo mizuri yakuwalinda wafanyakazi juu ya ajali na magonjwa sehemu za kazi.

Wamesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa mpana juu ya masuala ya usalama na afya, vitu ambavyo walikuwa hawavifahamu.

“Kama mwajiri atatekeleza kama ambavyo vision zero inataka, kuondoa magonjwa na ajali sehemu za kazi, nakama tutafuata maelekezo, natumaini tutaongeza uzalishaji sehemu za kazi na hivyo kuongeza pato la taifa.

“Kwani ukisema umeondoa ajali na magonjwa sehemu za kazi , hata wafanyakazi watakuwa na moyo wakufanya kazi zaidi na pia watakuwa na nguvu za kufanyakazi zaidi.

“Tutawashawishi waajiri wetu watekeleze kama ambavyo lengo kubwa la Vision Zero linataka”amesema Mvamila ambaye ni Mwakilishiwa kiwanda cha TPC Moshi.

Vision zero ni Kampeni ya Kidunia iiliyoanzishwa kwa lengo ya kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, kampeni hiyo inataka maeneo ya kazi kuwekwa mifumo ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi na kampeni hiyo inatekelezwa kwenye mataifa mbalimbali duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here