24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Waaandishi wa habari Simiyu wapewa vifaa kujikinga na Corona

Derick Milton, Simiyu

Waandishi wa habari Mkoa wa Simiyu wamepewa vifaa kinga mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Vifaa hivyo vimetolewa na mdau wa maendeleo katika Mkoa huo, ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyashimo Wilayani Busega Mickness Mahela ambapo amesema ametoa msaada huo kutokana na kazi kubwa wanayoifanya wanahabari nchini.

Vifaa hivyo vilivyotolewa na mdau huyo ni pamoja na vitakasa mikono (sanitizer), ndooo mbili za maji tiririka, sabuni za maji tano pamoja na barakoa zipatazo 46.

Mahela alisema kuwa wanahabari ni moja ya kundi ambalo lipo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa corona, hali ambayo imemfanya kutoa msaada huo.

” Tunajua wanahabari ni moja ya kundi kubwa, ambalo linakutana na watu mbalimbali na wako hatari zaidi kupata huu ugonjwa huu, mbali na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na corona, lakini wao wanatakiwa kuna na vifaa kujikinga,” amesema mahela.

Kiongozi huyo amewaomba wadau wengine kuungana naye katika kuwasaidia wanahabari kuwapatia vifaa hivyo kwani wengi hawana uwezo wa kuvipata, huku akieleza kuwa yuko tayari kutoa vifaa vingine kama vitaisha.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya waandishi wa habari Mkoani huo, Makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa Paschal Michael amemshukuru Diwani huyo kwa kutoa msaada huo.

Michael amesema kuwa Diwani huyo amefanya jambo kubwa na maana, kwani ni kweli wanahabari wako kwenye kundi hatari kutokana na kukutana na watu wengi zaidi.

” Tunakushukuru sana kwa msaada huu, tena umekuja katika wakati husika, ambapo Mkoa wetu nao umetangazwa kuwepo kwa mgonjwa mmoja wa Corona, mungu akubariki na kukuongezea pale ulipotoa,” alisema Michael.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles