27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

VYUO VYA ECKERNFORDE KUPIGWA MNADA

Jengo la Makao Makuu ya Taasisi ya Eckernforde lililopo katikati ya Jiji la Tanga linavyonekana.Pia katika jengo hilo kipo chuo cha walimu cha Eckernforde.

NA EVANS MAGEGE – DAR ES SALAAM

BENKI ya NBC imetangaza kuvipiga mnada shule na vyuo vya Eckernforde vya mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa tangazo la benki hiyo lililotolewa katikati ya wiki hii na Kampuni ya udalali ya Bani Investment Limited, Debt Collectors/Auctioneers na kuchapishwa katika magazeti mawili ya kila siku (si MTANZANIA Jumapili), limetanabaisha kuwa mnada wa chuo hicho pamoja na shule zake utafanywa Machi 11.

Akithibitisha taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Bani, Lita Colyvas, alisema taratibu za kutekeleza mnada wa vyuo vya Eckernforde umefuatwa kisheria.

“Ni kweli sisi ndio tumetangaza mnada huo kwa niaba ya Benki ya NBC, tumetoa tangazo siku 14 kabla ya mnada na siku tatu kabla ya mnada tutatangaza tena, ikiwapo kupitisha gari la matangazo mtaani,” alisema Colyvas.

Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni kile kilichojengwa kwenye kiwanja namba 53/2 na kiwanja namba 54/2, CT namba 2532, LO namba 62988, kitalu 111 chenye ukubwa wa mita za mraba 921 ambacho kipo eneo la Central Tanga.

Chuo kingine ni cha ualimu pamoja na sekondari ambacho kina ukubwa wa ekari 3,426 kwenye kiwanja namba 12, CT namba 18517, LO namba 170760 katika eneo la Kange Tanga.

Alisema kuwa vyuo hivyo vinatambulika kwa jina la Eckernforde Education Company Limited.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles