30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VINAVYOONGOZA KWA WANAFUNZI WAKE KUJIHUSISHA NA NGONO

KUFANYA ngono ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu hasa wakiwa maeneo ya chuo.

Tabia ya kupenda vitendo vya ngono vimeshamiri kwa wanafunzi vyuoni ukiachana tabia za utumiaji wa pombe na dawa za kulevya au uvutaji wa sigara.

Kufanya mapenzi kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni vitendo vya kawaida katika vyuo vikuu duniani.

Kuna vyuo ambavyo vitendo hivi vimekithiri zaidi, kujihusisha na ngono katika maisha yao ya kila siku wakiwa masomoni ni jambo la kawaida mno.

Baadhi ya vyuo vikuu nchini Marekani, wanafunzi wanaongoza katika kufanya vitendo vya kujamiana wakiwa maeneo ya chuo.

Kwa mujibu wa utafiti wa mtandao wa College Stats nchini Marekani, Chuo Kikuu cha Temple kinaongoza kwa wanafunzi wake kufanya vitendo vya ngono wakiwa kampasi.

Uchunguzi  uliyofanywa ulitumia njia ya kipekee ili kupata matokeo halisi katika kila chuo.

Wanafunzi 2,000 wapya na wa zamani, waliulizwa juu ya vitendo vya kujamiiana kwa wanafunzi ili kupata jumla ya wapenzi wao ambao wanashirikiana kingono.

Utafiti wa College Stats unasema waliangalia uhusiano na idadi ya wapenzi walionao ikijumlisha wapenzi wa wapenzi wao.

Chuo cha Temple ambacho kina wanafunzi 38, 297; kinashika nafasi ya kwanza kwa wanafunzi wake kufanya vitendo vya ngono kati ya vyuo vyote vikuu.

Chuo cha Rutgers kinafuatia, wakati nafasi ya tatu imeshikwa na Chuo Kikuu cha Cornell na Florida. Huku Pennsylvania kikishika mkia.

Uchunguzi ulibaini kuwa wanaume walikuwa na wastani wa wapenzi wa kingono 14 wakati wanawake walikuwa na wapenzi wasiozidi 12.

Hata hivyo, wanaume na wanawake kwa pamoja walionesha kufanya vitendo vya ngono kwa kiwango sawa kwa wastani wa watu tano.

Kwa upande mwingine, asilimia 43 ya wanawake wapenzi wao ambao walikuwa nao katika uhusiano walitokea chuoni hapo, wakati asilimia 35 ya wanaume wapenzi wao walitokea nje ya chuo.

Pia ripoti hiyo ilionesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hutumia kinga ya kondomu wakati wa kufanya mapenzi, tofauti na fikra za watu wengi, kwamba huenda hawatumii kinga.

Asilimia 38 ya wanafunzi walijibu kuwa wanatumia kinga kila wanapokutana kushiriki tendo, asilimia 24 walikuwa wanatumia mara chache wakati asilimia 15 hawatumii kabisa.

Aidha, asilimia 14 walikuwa wanatumia kulingana na mazingira, wakati asilimia nne walikuwa wanatumia pindi mwenza anapoomba.

Utafiti huo pia ulielezea kuwa matumizi ya kinga mara kwa mara kwa wanawake na wanaume ilikuwa asilimia 50 kwa 50.

Asilimia 75 ya wanaume hutumia kinga kama wakiombwa na wenza wao kufanya hivyo. Asilimia 35 ya wanawake walikuwa watumia kinga kama zikiwapo ambapo wanaume ilikuwa asilimia 65.

Kwa ujumla asilimia 15 ya wanafunzi ambao walijibu kuwa hawatumii kondomu walikuwa na wapenzi wanaokaribia wastani wa 18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles