Na Joseph Lino
KUNA vyuo vingi ambavyo vinatoa masomo ya udaktari katika maeneo mbalimbali ulimwenguni, lakini vyuo hivyo vinatofautiana ubora na uwezo.
Wanafunzi ambao wanahitaji kusoma udaktari katika vyuo vya nje ni lazima waangalie sifa za chuo husika.
Taasisi ya Times Higher Education ilitoa orodha ya vyuo bora duniani katika masomo ya udaktari ambavyo wanafunzi wanaweza kunufaika zaidi.
Lakini kusomea udaktari kuna tofautiana na nchi kulingana na utaratibu mbalimbali wa taaluma hiyo.
Orodha ya Times Higher Education ya vyuo bora 100 kutoka nchi 20 duniani kote inawapa mwanga wanafunzi wa taalamu hiyo ili waweza kuvijua vyuo vyenye ubora wa elimu.
Hii ni orodha ya vyuo vikuu tano bora ulimwenguni katika masomo mbalimbali ya udaktari.
Chuo Kuu cha Oxford, Uingereza
Masomo ya udaktari katika chuo cha Oxford nchini Uingereza hutoa kozi ya kliniki ambayo imegawanyika pande mbili (pre-clinical na clinical stages).
Miaka ya mwanzo mwanafunzi kuwa darasani kwa muda mrefu na baada ya miaka kadhaa huwa katika Clinical Stage ambapo kuwa na muda mwingi wa vitendo katika hospatali ya John Radcliffe nchini humo.
Takribani wanafunzi 150 hujiunga na kozi hiyo kila mwaka na wanafunzi 30 kuhitimu kila mwaka katika ngazi shahada ya udaktari.
Kujiunga katika kozi ya udaktari chuo cha Oxford mwanafunzi hufanya usahili ambao unakuwa wa ushindani, kwa mfano mwaka 2015 ambapo asilimia 11 tu walifaulu mtihani wa kujiunga na chuo hicho.
Chuo cha Harvard, Marekani
Chuo cha Harvard kilianzisha mwaka 1782 hufundisha taaluma ya udaktari kupitia idara ya sayansi, pia wanatumia hospitali nne ambazo zipo katika mji wa Boston.
Aidha, hutoa kozi maalumu (specialized program) ambapo wanafunzi 30 tu hukubaliwa kujiunga na kozi hizo ambazo zinalenga katika utafiti wa dawa za magonjwa (biomedical).
Cambridge, Uingereza
Chuo cha Cambridge hutoa kozi ya udaktari na kusajili wanafunzi 260 kwa ujumla.
Nusu ya wanafunzi wanaohitimu Cambridge wa shahada wanakuwa wataalamu hasa kwani hufanyakazi na National Health Service nchini humo.
Kujiunga na shahada ya udaktari unahitaji uwe umefaulu vizuri elimu ya sekondari na alama za juu
Imperial, Uingereza
Wanafunzi wa kozi ya udaktari mwaka wa kwanza, hufanya mazoezi na wagonjwa ikilinganishwa na vyuo vingine ambavyo hawafanyi hivyo.
Kozi ya udaktari huchukua miaka sita katika ngazi ya shahada kama vyuo vya Oxford na Cambridge, masomo ya udaktari katika chuo cha Imperial hujikita katika masomo ya sayansi na utafiti.
Wanafunzi wanaojiunga na kozi hiyo wanahitaji wawe na alama za juu kwenye masomo ya Sayansi na Kemia pamoja na kufuzu usaili.
Chuo cha Imperial ni miongoni mwa vyuo vya kimataifa lakini wanafunzi wachache hukubaliwa katika kozi ya udaktari kila mwaka.
 Chuo cha California na Berkeley, Marekani
Masomo ya kozi ya udaktari katika chuo cha California wanashirikiana na chuo cha Berkeley.
Vyuo viwili hivi vya umma hushirikiana kutoa taaluma ya udaktari darasani na utafiti.
Masomo hayo huchukua miaka mitano kuhitimu shahada ya udaktari, pia mwanafunzi hupata shahada ya uzamili katika afya ya jamii.