26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VIKUU VIDOGO BORA DUNIANI 2017

Chuo Kikuu cha École Normale Supérieure nchini Ufaransa

NA JOSEPH LINO,

WANAFUNZI wengi wa kimataifa mara nyingi huangalia orodha ya vyuo vikuu bora duniani ili kujua masuala mbalimbali hasa uwezo wa kufundisha masomo ya kitaaluma.

Pia wanaangalia uwezo wa chuo katika wingi wa wanafunzi, ukubwa wa kampasi na mambo yenye kuvutia.

Lakini kuna vigezo ambavyo hutumika katika kuchagua vyuo bora duniani kila mwaka, ikiwamo kufundisha kozi zaidi ya nne na kuwa na wanafunzi wasiopungua chini ya 5,000.

Wanafunzi wa kimataifa hutamani zaidi chuo chenye kampasi kubwa, kinachojulikana kwa shughuli mbalimbali za taaluma, pia wengi huvutiwa na uzoefu wa ufundishaji.

Hata hivyo, kuna vyuo vidogo duniani ambavyo havijulikani vizuri katika ramani ya elimu ya juu lakini vinatoa elimu ya juu katika kiwango bora kabisa.

Taasisi ya Times Higher Education imebainisha vyuo vidogo bora duniani ambapo walisikiliza maoni kutoka kwa wanafunzi wenyewe baada ya kuulizwa kitu gani wanapendelea katika kusoma vyuo vidogo.

Baadhi yao walisema kuwa kwa sababu ya madarasa madogo na kuwapo na ukaribu wa kimasomo na walimu.

Aidha, wanafunzi wa kimataifa waliosomo vyuo vikuu vidogo vilivyopo katika miji mikubwa walisema walifurahia mazingira ya chuo zaidi  na harakati za shughuli za maisha ya kila siku ya mji mkuu.

Wastani wa wanafunzi katika kila chuo kwenye ordha ya vyuo vidogo bora kwa mwaka 2017 ni 3,038, ikilinganishwa na wastani wa vyuo vikuu bora vikubwa ambayo ni 24,953.

Kwa wale wanaotamani kusoma nje kuna vyuo vikuu vidogo ambavyo havijulikani lakini ni bora zaidi katika kukuuza taaluma.

Orodha ya hivi karibuni inatoa nafasi kwa wanafunzi wa kimataifa ambao wanaweza kwenda kusoma katika vyuo vidogo bila kuwa hofu.  

Mwaka huu kuna baadhi vyuo vikuu vidogo vizuri ambavyo unaweza kusoma na kupata matokeo chanya.

Chuo cha California Institute of Technology (Caltech), Marekani

Chuo kikuu cha Caltech kimekuwa katika nafasi ya kwanza na kina mazingira mazuri ya kimasomo kwa miaka kadhaa mfululizo kina wanafunzi 2,000.

Kwa mujibu wa wanataaluma nafasi ya walimu na wanafunzi wa chache inaleta fursa ya majadiliano kwa upana katika chuo hicho.

Caltech kinatoa masomo katika taaluma ya sayansi na teknolijia ambayo yanafundishwa na maprofesa nguli.

 

École Normale Supérieure, Ufaransa

Chuo Kikuu cha École Normale Supérieure mjini Paris bado kinaendelea katika kushika nafasi ya pili. 

Chuo hicho kina wanafunzi 1,500, ambapo wanafunzi hupata uzoefu wa taaluma na mazingira bora ya mji.

Chuo hicho kinatoa fursa mbalimbali katika taaluma ya madawa na uhandisi.

 

Chuo cha Sayansi na Tekinolojia (POSTECH), Korea Kusini

POSTECH kilianzishwa mwaka 1986, kwa sababu ya ubora wake kila mwaka kudahili wanafunzi 320 katika njia maalumu ya usaili. 

Wanafunzi wa chuo hicho wanasifia madarasa yake madogo na kina maprofesa wanawajua kwa majina kila mwanafunzi.  

École Polytechnique, Ufaransa

Chuo cha École Polytechnique  kipo katika ubora wake hivi karibuni kimezindua masomo ya shahada ya uzamivu katika baadhi ya masomo na pia mwaka huu kilianzisha masomo ya taaluma ya hesabu.

Scuola Normale Superiore di Pisa, Italia

Hiki ni chuo kingine cha Scuola Normale Superiore di Pisa ni kidogo na kina wanafunzi  545, kinatoa kozi mbalimbali katika masuala ya sayansi.

Lengo kuu la chuo lilikuwa na kutafuta uhusiano kati ya wanafunzi wa sayansi na masomo ya maliasili watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles