25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Vyuo vikuu bora duniani mwaka 2016/2017

chuo-kikuu-cha-oxfordNa FARAJA MASINDE

UTAFITI wa mwaka 2016/17 kuhusu vyuo vikuu bora duniani tayari umetangazwa mwezi huu rekodi nyingi zikiwekwa.

Chuo Kikuu cha Oxford, kimeibuka kidedea katika orodha hiyo iliyojumuhisha vyuo takribani 200 kutoka duniani kote.

Shirika linalojishughulisha na utafiti wa ubora wa elimu ya juu duniani la Times Higher Education katika utafiti wake wa miaka na miaka limekuwa ni mara ya kwanza kwa Chuo Kikuu cha Uingereza kuibuka kidedea.

Katika utafiti huo nafasi ya pili imechukuliwa na Chuo kikuu cha Califonia huku ile ya tatu ikienda kwa Chuo kikuu cha Stanford.

Kwa upande wa vyuo bora vilivyopenya kwenye orodha hiyo kutoka Afrika ni Chuo Kikuu cha Cape Town cha Afrika Kusini ambacho  kimeibuka cha kwanza kutoka Afrika.

Inadhihirisha umahiri wa taifa hilo ambalo vyuo vyake vikuu sita vipo katika nafasi za vyuo vikuu 15 bora kikiwemo Chuo cha Witwatersrand katika nafasi ya pili, Stellenbosch nafasi ya tatu, Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal katika nafasi ya tano na Chuo Kikuu cha Pretoria katika nafasi ya sita.

Chuo Kikuu cha Makerere cha Uganda ambacho kiko ndani ya Afrika Mashariki ndicho kilichofanikiwa kupenya kwenye orodha hiyo ukiacha vile vya Afrika Kusini, kikiwa katika nafasi ya nne.

Vyuo vingine ni Chuo Kikuu cha Ghana katika nafasi ya saba na kile cha Nairobi kwenye nafasi ya nane.

Utafiti huo wa THE umekuwa ukitoa orodha yake hiyo kwa kuzingatia vitu vingi kama vile mafunzo, utafiti na mtazamo wa kimaaifa, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network barani Afrika, anasema vyuo vikuu vinne vya Afrika ambavyo ni Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana vimedhihirisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti kwenye mataifa hayo.

“Tumeshuhudia ongezeko kubwa kwa wanafunzi wanaofaulu kwenye shahada ya uzamivu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliyopita,” anasema Cloete.

Orodha ya vyuo vikuu vilivyoshika nafasi ya kwanza mpaka 10

Namba moja ni Oxford cha Uingereza kikifuatiwa na California Institute of Technology wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Chuo Kikuu cha Stanford vyote kutoka Marekani.

Nafasi ya nne ni Chuo Kikuu cha Cambridge cha Uingereza, ya tano ni Massachusetts Institute of Technology cha Marekani na namba sita ni Harvard cha Marekani.

Chuo kikuu cha Princeton cha Marekani kimeshika nafasi ya saba, nafasi ya nane ni Imperial College London kutoka Uingereza, namba tisa ni ETH Zurich – Swiss Federal Institute of Technology Zurich cha Uswizi huku vikionekana vikisalia nafasi zilezile kama ilivyokuwa kwenye utafiti uliopita.

Nafasi ya 10 imechukuliwa na Chuo Kikuu cha California, Berkeley cha Marekani kilichokuwa katika nafasi ya 13 kwenye utafiti uliopita.

Hata hivyo kwenye orodha hiyo kuna sababu mbalimbali ambazo zimechangia vyuo hivyo kuwa kwenye nafasi zake hizo.

THE wanasema kuwa mfano Chuo Kikuu cha Oxford ambacho kimeibuka kidedea kinaelezwa kuwa ni kutokana na kujiimarisha zaidi kwenye utendaji wake ili kuhakikisha kinaziba mapengo ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya (EU).

Kasi hiyo ndiyo imefanya chuo hicho kuimarika kwa asilimia 20 zaidi ikilinganishwa na kipindi kabla ya Uingereza kujiondoa kwenye umoja huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,544FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles